Header Ads Widget

RAIS UTPC AWATAKA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAANDISHI WA HABARI KUBADILIKA KIUTENDAJI.

 



Na Amon Mtega_ Dare-es Salaam .


 RAIS wa Umoja wa vyama vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Deogratius Nsokolo amewataka Viongozi wa vyama vya waandishi (Press Club) kwenye mikoa yao  kuendelea kuimarisha umoja  kwa kushirikiana na wanachama ili kufikia malengo mbalimbali ya mabadiliko ya vyama hivyo.


Nsokolo ametoa wito huo kwa Viongozi hao wakati  akizungumza  kwenye mafunzo ya siku tatu  ambayo yamegawanywa katika maeneo mbalimbali (ZONE) yaliolenga kufanya mabadiliko ya kiutendaji katika suala zima la uwajibikaji.


Rais huyo akizungumza kwenye mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Mbezi Garden jijini Dare-es Salaam huku yakiwa yamehudhuliwa na Viongozi wa vyama vya waandishi wa habari kutoka mikoa ya Ruvuma,Dodoma,Mtwara na Lindi huku wa mikoa mingine wamepangiwa maeneo mengine amesema kuwa baadhi ya vyama vya waandishi wa habari hapa Nchini vinashindwa kupiga hatua ya kusongambele kutokana na Viongozi wao kutokuwashirikisha mambo mbalimbali  wanachama wao.



 Kiongozi huyo wa muunganiko wa vyama vya waandishi wa habari hapa Nchini amesema katika kipindi hiki ambacho yanaenda kufanyika mabadiliko ya kuongeza kasi ya kiutendaji  kwenye vyama hivyo kila kiongozi abadilike ili mkoa wake usiweze kuachwa nyuma kimaendeleo.


 Katika mafunzo hayo  ambayo pia yamelenga  kuibua miradi mbalimbali ya vyama hivyo ,yamefundishwa na Daniel Naila pamoja na Nice Alex ambapo mada zilizofanyika ni suala la utawala bora,na namna ya kutunza kumbukumbu za kifedha manunuzi na malipo kwenye vyama hivyo pamoja na uibuaji wa miradi.



Kwa upande wake Daniel Naila ambaye ametoa somo la utawala bora amesema kuwa baadhi ya Viongozi wa vyama vya waandishi wa habari bado hawajui namna ya utawala bora jambo ambalo hupelekea kugombana na wanachama wao na baadhi yao hutowana kwenye madaraka kabla ya ukomo wa uongozi wao.


 Mwezeshaji Naila amesema kuwa kama Viongozi watazingatia suala zima la utawala bora basi migogoro mbalimbali kwenye maeneo yao itapungua kwa asilimia kubwa tofauti na sasa.



Naye Nice Alex ambaye amefundisha somo la utunzaji wa kumbukumbu za kifedha na manunuzi amesema kuwa kumekuwepo na baadhi ya Viongozi wa waandishi wa habari wamekuwa hawazingatii namna ya kutunza kumbukumbu hizo na kupelekea baadhi yao kutuhumiwa kuwa ni wabadhilifu wa fedha za wanachama.


 Nice amefafanua kuwa kama Viongozi watazingatia utunzaji wa kumbukumbu za kifedha ni rahisi hata kupatiwa wafadhiri ambao watawezesha vyama hivyo kuwa na maendeleo zaidi.


       

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI