Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Zaidi ya Hekta laki moja za Miti yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 400 zimeteketea kwa moto katika kipindi Cha miaka mitatu kutokana na sababu mbalimbali mkoani Njombe.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka katika kikao kazi kilichowakutanisha maofisa misitu,Zimamoto na Viongozi mbalimbali amesema ni lazima hatua za haraka zichukuliwe ili kukabiliana na majanga ya moto yanayosabisha hasara kubwa .
Mtaka amesema kila wilaya ikaweke mikakati ya pamoja kwa kuvifikia vijiji vyote kwa ajili ya kutoa elimu ya kukabiliana na matukio ya moto yanayoteketeza maelfu ya misitu.
Aidha Matukio 51 ya moto yaliyoripotiwa katika wilaya ya Njombe katika kipindi cha mwaka 2020/2021 yamesababisha hasara ya zaidi ya bilioni 200 kwa wananchi na misitu ya serikali.
Visasi na chuki pia ni miongoni mwa sababu zilizotajwa na wakala wa misitu Tanzania TFS wilaya ya Njombe Audatus Kashamakula licha ya kuwapo kwa sababu nyingine zikiwemo za ulinaji asali na uandaaji mashamba.
Joel Mwakanyasa toka jeshi la zimamoto mkoa wa Njombe anasema ipo haja ya kutoa elimu kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye mabaraza ya madiwani na mikusanyiko mbalimbali ya watu.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amekiri kupokea maelekezo yote ya mkuu wa mkoa na kuahidi kwenda kuyatekeleza kuanzia juma tatu ya Novemba 7 mwaka huu.
0 Comments