Header Ads Widget

KAMPENI YA TWENZETU KILELENI 'SEASON 2' YAZINDULIWA MKOANI KILIMANJARO



Na Esther Machangu


Uzinduzi ambao Umefanyika Leo Nov  9,2022 umeendana na kampeni ya upandaji wa miti elfu Tano ambayo imetolewa na kampuni ya Utalii Zara Tours,Umefanyika Mkoani Kilimanjaro.


Mkuu wa Wilaya ya Moshi Abbas Kayanda amesema  malengo ya kupanda mlima kilimanjaro ni pamoja na kumbukizi ya siku ya uhuru wa Tanzania ambapo kwa mara ya kwanza Bendera ya Tanzania ilipeperuka juu ya Mlima huo mrefu barani Afrika.


Kayanda ameongeza kuwa Malengo mengine ni kuhamasisha Utalii wa ndani,kuendeleza kampeni ya upandaji miti katika katika maeneo ya Mlima huo, na pia katika kipindi hiki Cha kampeni ya Twenzetu Kileleni gharama zimepunguzwa.

 


Naye Mhifadhi mwandamizi hifadhi ya Taifa ya mlima Kilimanjaro Charles Ngendo amesema hifadhi hiyo imejipanga kupokea na kuwahudumia wageni wote watakaokuja kupanda Mlima Kilimanjaro.


Afisa uhifadhi mwandamizi kutoka idara ya Mawasiliano, Catherine Mbena,amesema ni vyema watu watakaoenda kupanda Mlima kujiandaa kwa kufanya mazoezi ya pumzi Ili kukabuliana na Changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa.



Katibu wa Ccm wilaya ya Moshi Ibrahim Mjanakheri, amesema kutokana na kampeni ya Royal Tour iliyozinduliwa na Rais Samia Suluhu imeleta matokeo chanya katika sekta ya Utalii.


Kauli mbiu ya kampeni ya "TWENZENTU KILELENI SEASON TWO" Inasema otesha miti Kilimanjaro okoa maisha nusuru Utalii.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS