RAIS wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Deogratias Nsokolo
NA MATUKIO DAIMA APP DARRAIS wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Deogratias Nsokolo amewakumbusha waandishi kuacha kuandika habari za kusifia viongozi kwani hazina maslahi kwa umma.
Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Klabu ya waandishi wa Habari wa jiji la Dar es Salaam leo Novemba 6, 2022, Nsokolo amesema badala ya kusifia viongozi wa Serikali badala yake wafichue changamoto zinazowakabili wananchi.
Rais huyo wa UTPC amesema waandishi wamekuwa wakiandika habari za kusifia watawala badala ya kuandika yale yanayowagusa wananchi.
Nsokolo amesema waandishi watumie kalamu zao kuielezea Serikali matatizo yaliyopo ili iyatafutie ufumbuzi.
"Kwa mfano Serikali imejenga madarasa lakini madawati hayatoshelezi walimu wa masomo ya sayansi ni wachache na nyumba za walimu hakuna.
''Sisi ni sauti ya wasiokuwa na sauti tusizitegemee mamlaka kwani matatizo bado yapo Serikali inatekeleza wajibu wake hivyo tunaipenda Serikali yetu tunatakiwa tuieleze changamoto zilizopo kwenye jamii ili zifanyiwe kazi."amesema Nsokolo
Katika hali hiyo, Nsokolo ametolea mfano Mkoa wa Kigoma kwamba hakuna meli kwa muda mrefu katika Ziwa Tanganyika.
Kwa upande wake Mwenyeiti wa DCPC Samson Kamalamo, alisema klabu hiyo inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa vifaa vya ofisi, hivyo amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia ili kuboresha ofisi yao.
Wakati huo huo Meneja wa Mawasiliano Tanzania(TCRA), Semu Mwakyanjala amesema matumizi ya intaneti Tanzania yameongezeka kwa asilimia 4.2 kutoka 29,858,759,204 kwa mwaka 2021 hadi kufikia 31,122,163 kufikia Septemba mwaka 2022.
Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Rajabu Kinande ameshauri wanachama wanaokaribia kustaafu waanze kushughulikia mafao yao miezi sita kabla ya muda rasmi wa kustaafu ili waweze kulipwa mapema pindi wanapistaafu rasmi.
"Kibali cha kustaafu mfanyakazi anapata miezi sita kabla ya kustaafu, hivyo tunawasihi kushughulikia nyaraka zao kuondoa uchelewaji wa kupata mafao yao kwa wakati."amesema bosi huyo wa PSSSF.
0 Comments