Na Elizabeth Ntambala, Matukio DaimaAPP Rukwa
Wananchi wa kijiji cha Nambogo Manispaa ya Sumbawanga wameishukuru serikali ya Awamu ya Sita kwa kusaidia kukamilisha ujenzi wa zahanati yao iliyoanza kujengwa mwaka 2000 na kukamilika mwaka huu.
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa zahanati hii leo kwa niaba ya wananchi Mzee Lemeli Mbalamwezi (86) ambaye ndiye alitoa eneo hilo alisema wanaishukuru serikali kwa kutoa fedha zilizosaidia mradi huo.
“Tunashukuru viongozi wa chama na serikali kwa kutujengea jengo la zahanati hapa Nambogo na sasa tusaidiwe kupata shule ya sekondari karibu na kijiji chetu”alisema Mzee Mbalamwezi.
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga alisema alisema anamshukuru Rais Samia Suluhu Hasan kwa kutoa fedha pia kumwamini na kumteua kufanya kazi Rukwa ambapo atahakikisha hakuna miradi viporo inasalia.
0 Comments