NA TITUS MWOMBEKI, Matukio Daima App Kagera
MKUU wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila ameagiza Wakala wa ujenzi wa barabara mjini na vijijini (TARURA)kuanza utekelezaji wa ujenzi wa barabara Nyamkazi ili kuwasaidia wakazi wa mtaa huo ambao kwa wingi wao ni wavuvi kuondokana na changamoto hiyo
Ameyasema hayo leo Novemba 10,2022 alipokwenda kukagua barabara hiyo akimbatana na viongozi mbalimbali wa mkoa pamoja na mtaa huo baada ya wavuvi hao kuomba barabara hiyo itengenezwe ili kurahisisha mawasiliano.
"Jana nikiwa hapa wenzetu wakazi wa mtaa huu waliomba barabara hii itengenezwe ili waweze kufanya shughuli zao kwa urahisi katika mtaa huu, sasa nimekuja na viongozi wa TARURA waweze kuiangalia na matengenezo yaanze mara moja" R.C Chalamila.
Kwa upande wake Katibu Tawala mkoa wa Kagera, Toba Nguvila ameongeza kuwa kilio cha wavuvi kimesikilizwa huku akiwasihi waendelee kufanya shughuli zao uvuvi kwa njia ambazo sio haramu.
Naye meneja wa TARURA katika Manispaa ya Bukoba, mhandisi Avith Theodory amesema kuwa wameyapokea maagizo hayo huku akisema kuwa kazi ya kufanya matengenezo itaanza hivi punde na inategemewa kutumia mwezi mmoja itakuwa imeishakamilika.
0 Comments