Na Scolastica Msewa, Dar
Shirika la Uhifadhi wa Mazingira duniani , WWF Tanzania imewajengea uwezo taasisi za fedha ambazo wanachama wa umoja wa mabenki Tanzania (TBA) kwa lengo la kuhakikisha utoaji wa huduma za kifedha endelevu unaozingatia utunzaji wa mazingira, kuhusisha jamii pamoja na ukuaji wa uchumi, washiriki wa mafunzo haya zaidi ya benki 44 ambao ni wanachama wa Umoja wa Mabenki Tanzania
Akizungumzia na Waandishi wa Habari kwenye mkutano wakuzijengea uwezo benki Afisa Miradi wa WWF Tanzania Happiness Minja katika warsha iliyofanyika Protea Hotel jijini Dar es salaam alisema Mkutano huo unawajengea uwezo wa kuwa na tahadhari za utunzaji wa mazingira, masuala ya kijamii na kuzingatia ukuaji wa uchumi kwa mikopo na mawasiliano ya wawekezaji katika benki wanapoomba mikopo
Alisema benki wanapotoa mikopo kwa wawekezaji wa ndani na wa nje ya nchi wazingatie miradi inayolinda na kutunza mazingira, kujali jamii na kuzingatia suala la ukuaji wa uchumi wa nchi na sio inayochochea uharibifu wa mazingira nchini.
Alisema benki wasitoe mikopo kwa kuangalia kupata Wateja wengi wa mikopo bali pia wahakiki na wateja wao watazingatia utunzaji wa mazingira katika Uwekezaji wao kwenye jamii nchini.
0 Comments