*********************
NA TITUS MWOMBEKI, Matukio Daima App Kagera.
WIZARA ya Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu imejitolea kuwasaidia wasanii wenye ulemavu waliotumbuiza katika sherehe kilele cha mbio za mwenye wa uhuru mkoani Kagera ikiwa ni njia ya kutambua kazi zinafonywa na waanii wenye ulemavu mkoani humo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako baada ya wasani hao wenye ulemavu waliotambulika kwa jina la Novath Mwesiga ambaye ni msanii na mtunzi wa shairi pamoja na Albert Christian kumaliza kutumbuiza mbele ya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alikuwa mgeni rasmi sherehe hizo.
“Tunatambua kazi zinazofanywa na wenzetu wenye ulemavu katika jamii na Taifa kwa Ujumla hivyo basi ndugu zetu hawa waliotumbuiza na kutuburudisha leo kupitia wizara ninayoisimamia mimi tutawawezesha kurekodi nyimbo zao bure ikiwa ni njia mojawapo ya kutambua mchango wao katika jamii” alisema Prof.Ndalichako.
Kwa upande wake Novath Mwesiga amemshukuru waziri Joyce Ndalichako kwa kuweza kutambua kazi zao na kuwahaidi kuwawezesha kurekodi kazi zao suala ambalo kwao kama wasanii lilikuwa likiwapa changamoto katika kufanya kazi zao.
“Tunamshuru waziri kwa kuona umuhimu wa kazi zetu kama wasanii wenye ulemavu na kuhaidi kutuwezesha kurekodi nyimbo zetu bure, tulikuwa tunapata changamoto kubwa hasa ya kifedha katika kurekodi nyimbo zetu ili ziweze kudumu na kuingia sokoni hivyo kupitia ahadi aliyoitoa waziri wetu inatupa hamasa kuendelea kutunga nyimbo pamoja na mashairi yenye lengo ya kuelimisha na kuburudisha jamii” alisema Mwesiga.
Sambamba na hilo ameiomba jamii mkoani Kagera kuendelea kutambua kazi zinaofanywa na watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kuwaunga mkono wanapohitaji msaada wao hata wa kimawazo.







0 Comments