Header Ads Widget

WESE KUWAPA SHAVU MADEREVA BAJAJI NA PIKIPIKI

 


Na fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe leo amezindua Kampuni ya Wese ambayo inalengo la kuwasaidia vijana waendesha bodaboda na bajaji kuweza kupata mafuta kwa njia ya mkopo na kulipa baadae Ili kuweza kujiendesha kiuchumi katika biashara zao.


Akizungumza na wadau mbalimbali wakati akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Gondwe ameipongeza kampuni hiyo kwa kuja na wazo hilo la kuweza kusaidia vijana wa kitanzania katika kuendesha biashara zao hasa pale wanapokuwa na vyombo vya moto ikiwemo bajaji na bodaboda 


"Hii ni fursa kwa vijana wa Dar es salaam, watu wengi wanaoendesha bajaji na boda boda sio za kwao, nijambo kubwa sana, wanakuja na changamoto ya mafuta lakini kupitia kampuni hii ya Wese, itakwenda kunufaisha watu wengi na wapenda maendeleo, "amesema Gondwe.



Amesema kuwa, kupitia application ambayo inawawezesha vijana hao kuweza kujiunga itawasaidia kuwatambulisha duniani kote na kuweza kupata kuaminika ndani na nje pamoja na kuweza kukopesheka kupitia kwenye mabenki.


"Kwa sababu mradi huu umeanzia Dar es salaam itakwenda mpaka Lagos Nigeria, south Afrika, katika mtazamo wa kiafrika na ningependa makao makuu yaweke kinondoni"amesema Gondwe..


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mwanzilishi  Kampuni ya Wese Francis Ekeng  amesema kuwa Sekta ya Uchukuzi nchini Tanzania ni moja wapo ya waajiri wakubwa wa wafanya kazi kwa sababu ya nafasi yake ya kimkakati katika kukuza uchumi wa Taifa.



Aidha, amesema kuwa Wese itakua Jukwaa la kwanza la kiteknolojia ambalo limeanzishwa nchini Tanzania lilotafitiwa nchini Tanzania, kuendelezwa nchini Tanzania na vijana wenye hakimiliki nchini Tanzania na kuzinduliwa na kupelekwa nchi nyengine barani Afrika na kwimgineko.


"Tukiwa pamoja na na mshirika wetu, benki ya Equity, tunawahakikishia watanzania kwamba makao makuu ya Wese yatakua Tanzania Taima, bila kujali ukuaji wetu, wakati tunajenga Thamani ya madereva, tuligundua kwamba tumejenga Thamani ya juu kwa vituo vya kujaza mafuta na wamiliki wao"amesema Ekeng. 



Amesema kuwa, wanafanya kazi kama mawakala wa mauzi na masoko ambao hununua mafuta kwa wingi kutoka kwenye bohari zao,ambapo halu hiyo itapungiza gharama za uhifadhi wa mafuta kwenye bohari huku ikiongeza kwa kiasi cha mauzo yao na hisa za soko kwa vituo vya washirika.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS