Header Ads Widget

WAZAZI WENYE WATOTO WENYE USONGI, MTINDIO WA UBONGO WAMEOMBWA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE

NA TITUS MWOMBEKI, Matukio Daima App Kagera.

WAZAZI wenye watoto wenye ulemavu wa akili pamoja usonji mkoani Kagera wameombwa kuendelea kuwapeleka watoto wao katika shule maalumu zilizotengwa kwa ajili yao ili kuweza kupata elimu.



Hayo yamesemwa na afisa elimu msingi Manispaa ya Bukoba, Maseke Sheja  ambapo amesema kuwa serikali inaendelea kuboresha mazingira ili kila mtu anafanikiwa kupata elimu hapa nchini bila kubaguliwa.


“Dunia sasa hivi imeisha badilika kila mtoto anaweza kupata elimu bila kujali ni mwenye changamoto ya usikivu, uoni hafifu, mtindio wa ubongo au mwenye ualbino wote hawa wana namna ya kuelimishwa ndiyo maana serikali imeanzisha elimu jumuhishi hivyo wazazi hawatakiwi kuwaficha watoto wao wawapeleke shule wapate elimu”


Ameongeza kuwa katika Manispaa ya Bukoba kuna shule tatu za msingi  zinatoa elimu maalumu kwa watoto wa kundi hilo maalumu ambazo ni shule ya Msingi Tumaini, Mgeza Mseto pamoja Mzeza viziwi huku amkiwasisitiza wazazi wenye watoto wenye ulemavu kuwapeleka watoto wao katika shule hizo na kuachana na dhana potofu ya kusema kuwa watoto wenye ulemavu hawafundiki.


Kwa upande wake mwalimu John John anayefundisha shule ya msingi Tumaini kitengo cha watoto wenye mtindio wa ubongo na usonji amesema kuwa wamekuwa wakipokea wanafunzi wengine kutoka nje ya Manispaa ya Bukoba huku akisisitiza kuwa kutokana na elimu inayotolewa hapo imewasaidia watoto wenye changamoto ya mtindio wa ubongo pamoja na usonji kujua kusoma na kuandika pamoja na kuchangamka.



“Watoto mara nyingi wanakuwa na changamoto ya upokeaji na uwasilishaji wa taarifa, sisi katika ufundishaji wetu tunaanza na shida kubwa ambayo mtoto anasumbuka nayo ndiyo tunayoansha kushughulikana nayo hapa kuna watoto walikuja hawawezi kufanya kitu chotote tukawafundisha na sasa hivi wanaweza kufanya baadhi ya vitu mfano kuandika, kusoma wenygine wanaweza kujiosha opamoja na kusukutua meno lakini hapo awali walikuwa awawezi kabisa”


Aidha amewasihi wazazi pamoja na wana habari kuendelea kuhamasishana hususa ni kwa wazazi wenye wato wenye ulemavu kuendelea kuwapeleka watoto wao katika shule hizo hata kama watoto hao wanapatikana je ya manispaa ya Bukoba anaweza akawasiliana na ndugu ambaye anakaa Manispaa ili mtoto apate pa kufikia akiwa anatoka shuleni hapo kwani shule hiyo sio ya bweni.


Naye Akastazia Komugisha mwenye mtoto mwenye mtindio wa Ubongo  anayesoma katika Shule ya Msingi Tumani ameishukuru serikali kwa kuendealea kutimiza jukumu la kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bila kujali changamoto walizo nazo huku akielezea jinsi elimu jumuishi ilivyomsaidia mtoto wake.


“Mwanangu alikuwa awezi kuchangamana na wenzake, huwezi kumtuma kitu Fulani akaleta mpaka sasa namshukuru Mungu nilipompeleka shuleni hapo kwasasa walau anachangamka hata kama sio sana lakini angalau sio kama alivyokuwa zamani”


Aidha ameiomba serikali kuendelea kutoa elimu kupitia vyombo vya habari kuelimisha jamii hasa watu wa vijjini ambao kwa wingi unakuta watoto wenye changamoto kama hizo wanapatikana hukio ili ijue kuwa kuna shule maalumu zinazotoa elimu kwa watoto wenye ulemavu hapa mkoani Kagera.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI