Header Ads Widget

WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA MICHEZO

Afisa Michezo Mkoa wa Tabora, Katuli Hassani akizungumza na alaiki ya watu katika uwanja wa mpira wa Ali Hasani Mwinyi mkoani Tabora .

Watoto waliohudhuria kumbukizi za mwalimu nyerere mkoani Tabora
Mratibu wa chama cha Riadha mkoani Tabora Allan Ntana akizungumza na wananchi mkoani Tabora 

                                xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Lucas Raphael,Tabora

 

 Afisa Michezo Mkoa wa Tabora, Katuli Hassani   amewamasisha wananchi kutumia fursa za michezo ili kuinua uchumi na kujenga afya zao.

 

Kauli hiyo imetolewa leo kwenye viwanja vya Alli Hassani Mwinyi wakati akizindua michezo ya mbio za baiskeli kuadhimisha siku ya  kumbukizi ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere .

 

Afisa michezo huyo alisema kwamba wananchi watumie fursa za michezo mbalimbali inayofanyika mkoani hapa.

 

Maadhimisho hayo alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Batrida Buriani ambaye alisema kwamba wananchi wanapaswa kujitokeza kwenye mazoezi mara kwa mara ili kujenga afya zao.

 

Aidha alisema katika kuadhimisha kumbukizi hiyo kupitia michezo mbalimbali ilifanyika ya mashindano ya baiskeli, mbio za kawaida na kuweza kupata washindi kutoka mkoani hapa.

 

Aliwataja washindi hao wa baiskeli kundi (a) Masunga Mrisho, (b) Rajabu Issa (c) Samweli Mussa ambapo kwa sasa waliweza kuchuja na kupata mmoja ambaye atakaye wakilisha mkoa wa Tabora.

 

Mashindano mengine ya mbio za kawaida kwa wanafunzi wa shule za msingi mkoani hapa walioshinda mita 100 Frednand Lucas, Evodia Nasibu na Haruna Nasibu na wengine mita 4oo Jombo Hamisi, Evodia Nicas na mita 1,500 Mrisho Gambo, Masesa Juma na Bahati Dua.

 

Kwa upande wake mratibu wa chama cha Riadha mkoani Tabora Allan Ntana alisema kuadhimisha kumbukizi la hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere  ni kumkumbuka kwa jinsi alivyokuwa akipenda michezo ya aina mbalimbali ndani ya nchi na nje.

 

Alisema hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni muaasisi na alikuwa anaipigania nchi yetu enzi ya Uhuru na  mwana michezo.

 

Aidha Ntana alisema kwamba aliwapenda wananchi waliokuwa wakipenda mchezo wa jadi wa bao na kushiriki kwa wananchi katika mchezo huo.

 

Hata hivyo alisema hayati Mwalimj Julius Kambarage Nyerere alikuwa hapendi ubaguzi wa rangi wala kabila aliwapenda wananchi wake.

  

Amewahimiza vijana mkoani hapa kujitokeza kushiriki michezo mbalimbali ili kujenga afya zao na waweze kujipatia kipato

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI