**********************
Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam
Wananchi wa Mtaa wa Buguruni Kisiwani maarufu Ghana wamelipongeza jeshi la Polisi kwa kudhibiti vitendo vya kihalifu vinavyofanywa na panyaroad ambavyo vimekua vikiwaumizwa wananchi wengi wa mtaa huo.
Pongezi hizo wamezitoa jijini Dar es Salaam wakati walipokuwa katika Mkutano wa kutoa taarifa ya kazi kuanzia mwezi January hadi October mwaka huu ulioandaliwa na Mwenyekiti wa Serikali wa mtaa huo Uwesu Bakari Uwesi ambapo wananchi wameonekana kupendezwa na juhudi zinazofanywa na jeshi la Polisi.
Prisca Masanja ni miongoni mwa wananchi ambao wamelipongeza jeshi hilo, amesema katika Mtaa huo hali ilikua sio shwari hata kidogo kutokana na panyaroad walivyokuwa wakiwatesa kwa kuwapiga mapanga na kuwaibia vitu vyao majumbani mchana kweupe bila kujali chochote.
"Tunalishukuru jeshi la Polisi kwa kuwadhibiti wahalifu hawa, kwani hali haikua nzuri hata kidogo, tulikuwa tunaishi kwa hofu lakini nitowe wito kwa wazazi wasiwafiche watoto wao wahalifu wawafichue,wawasalimishe kituo cha Polisi, kwani wale ni wauwaji wanapokukuta watakuchukulia kila kitu na bado watakupiga tena vibaya"amesema Prisca.
Uwesu Bakari Uwesi ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa huo, amewataka wazazi na walezi kushirikiana na jeshi la Polisi katika kupambana na vitendo hivyo na endapo atapata taarifa kuwa mwanae ni muhalifu basi aliache jeshi la Polisi lichukue sheria na sio kukimbilia kituoni kumtoa.
"Jeshi la Polisi linajitoa sana kupambana na vitendo vya kihalifu mtaani kwetu hasa vinavyosababisha na panyaroad, lakini wazazi munalivunja nguvu kwa kukimbilia kituoni kuwatoa watoto wenu wanaapokamatwa,munawarudisha tena mtaani wanakuja tuumiza, mimi niliibiwa nyumbani kwangu mchana saa nane"amesema Uwesu.
Msahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto pia amelishukuru jeshi la Polisi chini ya usimamizi wa kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Muliro kuhakikisha wanawashughulikia wahalifu wote na kulifanya Jiji hilo kuwa katika hali usalama.
"Tumeskia taarifa hapa za wananchi walikuwa wanaishi kwa hofu sana kuwaogopa panyaroad kwani walikuwa hawawezi hata kwenda msikitini Sala ya alfajir, na wakiristo nao walikuwa wanashidwa kwenda ibada zao za mapema kwa kuhofia usalama wao"amesema Kumbilamoto.
Busoro Pazi ni Diwani wa Kata ya Buguruni ametoa rai kwa wananchi hao kwa kuwataka kuweka taa nje ya nyumba zao ikiwa ni njia ya kuimarisha ulinzi na usalama ili hata itakapotokea wahalifu wakatokea iwe ni rahisi kuwaona na kuwachukulia hatua.









0 Comments