Header Ads Widget

WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA WAMESHAURIWA KUANDAA MASHAMBA MAPEMA KABLA MSIMU WA KILIMO KUANZA.

 Afisa kilimo Mwandamizi na Mkaguzi wa Pamba wilaya ya Igunga Mkaoni Tabora Venas Kankutembe
 
                                         Masalia ya Pamba yakiteketezwa shambani

Baadhi ya wakulima wakioneshs namna ya kuondoa masalia ya Pamba shambani

                                xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Chausiku Said, Matukio DaimaApp.

Wakulima wa Pamba wametakiwa kuandaa mashamba mapema kabla ya msimu wa kupanda Haujafika kwa kufanya matayarisho ya kun'goa na kuchoma moto masalia ili kudhibiti mzunguko wa wadudu waharibifu wa zao Hilo pamoja na vimelea vya magonjwa.

Hayo yamebainishwa na Afisa kilimo Mwandamizi na Mkaguzi wa Pamba wilaya ya Igunga Mkaoni Tabora Venas Kankutembe na kusema kuwa wakulima anapaswa kuandaa mashamba mwezi mmoja kabla ya kuanza msimu wa kilimo.

Venas amesema kuwa wakulima wanapoandaa  mashamba wanatakiwa kung'oa masalia kwa kuchimbua chini na kuondoa visiki kwani kwa kufanya hivyo atakuwa amepunguza ongezeko la wadudu ambao wangeweza kuzaliana kwenye masalia na kusababisha mashambulizi katika msimu unaofata.

"Visiki vikiachwa vitaota na kusababisha wadudu kuendelea kufanya mashambulizi na ndio maana tunawaimiza wakulima wanavyong'oa masalia waweze kutumia jembe kuondoa mche mzima pamoja na kuchoma moto" Alisema Venas.

Amefafanua kuwa wakulima wanapaswa kuzingatia kanuni za kuandaa Shamba mapaena na kwa ufasaha kwa kufanya hivyo kutawasaidia kupanda Pamba Mara tu baada ya mvua zitakapoanza kunyesha na sio kusuburi mvua ianze kunyesha ndipo wanaanza kuandaa mashamba Kwa kufanya hivyo watasababisha Pamba kutokuota Kwa wakati.

" Ili upande Pamba Kwa wakati na uvune wakati sahihi ni lazima kuandaa Shamba lako mapema, lakini sasa wapo wakulima wanamsubiri mvua inyeshe ndio waandae Shamba ndio maana unakuta mtu anatapa Pamba kinyume na matarajio aliyokuwa amejiwekea hiyo hayo yote yanatokana na ulimaji wa bila kufata maelekezo kutoka kwa watalamu wa kilimo" Alisema Venas.

Saizi Ngusa na Amos Makalanga Ni wakulima wa zao la Pamba wameeza kuwa Kuna umuhimu wa kuondoka masalia mashambani Mara baada ya kuvuna kwani Kwa kufanya hivyo kunawasaidia kuondoa wadudu waharibifu wa zao Hilo.

" Kwanza tukisha vuna Pamba alafu tukaondoa masalia shambani inatusaidia sana hususani katika msimu mwingine wa kilimo unapofika hatusumbuki sana kwa sababu Shamba linakuwa Safi" Walisema.

Wameeleza kuwa elimu waliyoipata Kwa sasa imewasaidia na kilimo kimebadilika tofauti na zamani mtu alikuwa akilima anaacha masalia ya miti ya Pamba kukua na kuanza kuchipua tena, na kusubilia parizi hali iliyopelekea kutopata Pamba yenye ubora.

" lakini kwa sasa tunapokata masalia ya Pamba na kuyateketeza Kwa moto ili kuweza kuwaangamiza wadudu waharibifu ili msimu ujao wasiweze kuaribu Pamba kumetusaidia sana na kuona kilimo Cha Pamba ni kizuri zaidi kuliko kilimo kingine" Walisema.














Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI