Header Ads Widget

"VIPENGELE VYA SHERIA YA HABARI VIBORESHWE" - BALILE

 


Na fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam


Imeelezwa kuwa, endapo vipengele vilivyopo kwenye sheria ya habari vitaweza kufanyiwa maboresho itamsaidia mwananchi kupata habari bila vikwazo vyotote.


Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile wakati alipokua katika mafunzo kwa waandishi wa habari ambapo amesema  maboresho ya sheria hiyo si kwa faida ya wanahabari pekee kupata uhuru wa kutoa na kupokea habari bali pia kwa wananchi ambao watapata habari na kutoa maoni kupitia vyombo vya habari.


"Tunaamini tunafanya swala hili kwa nia njema ya kuwawezesha watanzania kupata habari bila vikwazo na mwisho wa siku sio wanahabari peke yao watafurahia matunda ya kutoa na kupokea mawazo hata wananchi pia watafaidika" amesema Balile.


Aidha amesema haki inakuja na wajibu hivyo uhuru wa vyombo vya habari ukipatikana kwa mujibu wa sheria kama wanavyoomba ni lazima wanahabari kufanya kazi kwa kuzingatia misingi na weledi wa taaluma hiyo ili kulinda hadhi ya taaluma hiyo na wale wanaotoa taarifa kwenye mitandao ya kijamii.


"Taaluma ya uandishi wa habari haitakaa ife kama wengine wanavyoamini mitandao ya kijamii itaiua, endapo tutaifanya kazi kwa kuzingatia maadili na haki za wengine hii itaambukiza hata wale wa mitandao ya kijamii kuona kuna kitu cha ziada kilichopo kwenye uandishi wa habari"amesema Balile.


Hata hivyo, amesema tayari wameshakutana na Serikali, Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye kujadili maboresho ya baadhi ya vifungu katika sheria hiyo hivyo ni matumaini ya wanahabari kuwa Bunge la Novemba mwaka huu muswada wa mapendekezo ya mabadiliko /maboresho ya sheria hiyo utajadiliwa Bungeni.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI