Header Ads Widget

MAKANDARASI 18 WASAINI MKATABA RC ARUSHA ASISITIZA UZALENDO

 


Teddy Kilanga_ Matukio Daima APP-  Arusha


Serikali mkoani Arusha imewataka Makandarasi wa wa wakala wa barabara za vijijini  na mijini(Tarura) wanaotekeleza miradi mbalimbali mkoani humo yenye thamani  ya takribani sh.bilioni 18.2 kuimaliza kwa wakati ili wananchi waone tija ya uwekezaji wa fedha hizo.


Akizungumza katika hafla ya uingiaji wa mikataba kwa Makandarasi 18 ya awamu ya pili ulifanyikia jijini Arusha,Mkuu wa mkoa wa Arusha alisema serikali imetoa fedha hizo kwa ajili uboreshaji wa miundombinu ya barabara hivyo ni wajibu wao kuhakikisha inakamilika kwa wakati ili kukuza uchumi wa wananchi.


Hata hivyo Mkuu huyo alisisitiza Makandarasi waliopewa tenda ya utekelezaji wa miradi hiyo kuhakikisha ujenzi wake unatekelezwa kwa viwango vilivyopo kwenye mikataka yao.


"Barabara ni maendeleo kwani zinasaidia kukuza uchumi wananchi kutokana na miundombinu hiyo kupita inapunguzia wafanyabiashara mbalimbali gharama za uendeshaji wa biashara zao ikiwemo usafirishaji wa malighafi katika kufikisha sehemu ya uzalishaji,"alisema Mongela.


"Napenda kusisitiza Meneja wa Tarura na timj yako kwenda kusimamia miradi hii kwa karibu lakini Makandarasi tuongeze uzalendo kidogo kwani mmeaminiwa nyinyi wazawa katika utekelezaji huu,"alisema Mkuu wa mkoa huyo.



Kwa upande wake Meneja Tarura mkoa wa Arusha,Mhandisi Laynas Sanya alisema kwa mwaka wa fedha 2022/2023 walitengewa jumla ya kiasi cha sh.bilioni 18.2 kwa ajili ya matengenezo ya barabara ambapo kati ya hizo sh.bilioni 8.2 ni katika mfuko wa barabara wa miradi 29 ikiwa sh.bilioni 3.5 ni fedha za jimbo kwa ajili ya miradi saba huku sh.bilioni 6.5 ni nyongeza ya mafuta zitokanazo na tozo.


Mhandis Sanya alisema Tarura mkoa wa Arusha  iliweza kuingia  mikataba 34 awamu ya kwanza ya asilimia 60 yenye thamani ya sh.bilioni 14.3 ambapo sh.bilioni 7.2 ni fedha za mfuko wa barabara yenye jumla ya mikataba 18 na sh.bilioni 2.8 ni fedha za jimbo yenye mikataba saba ikiwa sh.bilioni 4.2 ni ya mikataba tisa zikiwa ni nyongeza  za mafuta kupitia tozo.


Alisema mikataba 18 ya awamu ya pili yenye takribani sh.bilioni nne ambapo sh.bilioni 2.4 ni fedha za mfuko wa barabara yenye mikataba 11 na sh.bilioni 1.6 yenye mikataba saba ikiwa ni fedha za tozo ya mafuta.


"Jumla ya mikataba 52 yenye jumla ya sh.bilioni 18.2 ikiwa katika mikataba hiyo iliyosainiwa ni za baadhi ya barabara zenye umuhimu mkubwa ikiwemo  pamoja na ujenzi wa sanduku la boksi katika barabara ya Njiro ndogo wilayani Arusha,kuchonga na kuweka changarawe katika barabara za Olturoto (Mringa 2700m³) ,"alisema.


Aliongeza kuwa nyingine ni pamoja na barabara ya oljoro,duka la mbao,Laroti 2700m³ wilayani Arumeru,ujenzi mwingine katika barabara ya Manyara Lositete wilayani Karatu sambamba na barabara ya Namanga Sinoniki wilagani Longido pia ujenzi wa sanduku la boksi katika barabara ya Lashaine Primary school wilayani Monduli pamoja na kuchonga na kuweka Changarawe katika barabara za Loliondo Tinaga 8400³ wilaya ya Ngorongoro.


Mmoja wa Makandarasi kutoka kampuni ya Lenana Holding LTD,Ally Tesha alisema wanaishukuru serikali kupitia Tarura mkoani Arusha kwa kuwaamini hivyo utekelezaji wa miradi utaenda kwa wakati ili malengo ya serikalo yatimie na uchumi wa wananchi uendelee kukua.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI