Header Ads Widget

TAYAC YAANZA MIKAKATI YA KUPUNGUZA CHANGAMOTO YA UHABA WA WANARIADHA

 


Teddy Kilanga Arusha

Kutokana na changamoto uhaba wa wanariadha nchini wazazi wametakiwa kuwa na tabia ya kuwapeleka watoto wao katika vituo vya riadha kwa ajili ya kupata wakimbiaji bora wa kizazi kipya watakaoleta ushindani katika michezo ya kimataifa.


Hayo yamebainishwa  katika mkutano wa waandishi wa habari katika kuelekea mashindano ya pili ya riadha yanayotarajiwa kufanyika Oktoba 15 hadi 16,2022 yaliyoandaliwa na Tanzania Youth Athletics Campionship(TAYAC), Kocha mkuu wa riadha nchini,Suleman Nyambui alisema wazazi wanao wajibu wa kuhamasisha mchezo huo kwa watoto wao ili kusaidia Taifa kupata wachezaji wengi zaidi.


Aidha Mwenyekiti huyo alisema hapo awali mwaka 1970 wachezaji wa riadha walikuwa wengi tofauti na kipindi cha sasa hivyo ni wakati wa kuhamasha vijana wapende mchezo huo ili nchi iweze kupata wawakilishi katika michezo ya kimataifa.


"Sasa hivi nchi ina upungufu mkubwa kwa wanariadha tofauti na nchi nyingine hivyo tunaomba wazazi wawatengenezee mazingira watoto wao kupenda mchezo wa riadha ikiwa kama sehemu ya ajira kwao pamoja na kujenga afya,"alisema Mwenyekiti huyo.


Katibu wa chama cha riadha mkoa wa Arusha,Rogath John alisema njia ya kupata wanariadha wengi nchini ni kuendelea kutoa elimu kwa wazazi na walezi kuhamasisha watoto wao kupenda mchezo huo ambao ni chachu katika kukuza uchumi wa Mwanariadha na kuletea heshima.


Awali akielezea mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Oktoba 15 hadi 16,2022,Msemaji wa TAYAC, Kasmiri Valentine alisema lengo ni kuhamasisha vijana  na watoto kushiriki katika mchezo huo ili kuweza kukuza vipaji vya nakuweza kufikia hatua za kimataifa ili kuweza kujikwamua kiuchumi.


"Mashindano hayo yatahusisha vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 20 ikiwa mpangilio wa mbio hizo umegawanywa kulingana na umri wao na michezo itakayohusika ni pamoja na mbio fupi za mita 100,200 na 400,"alisema Valentine.


Aliongeza kuwa mbio za kati ni za mita 800,1500 na 3000 na kwa upande wa vihunzi itakuwa ni za mita 100 ikiwa vijiti ni 4 kwa 100 mita na 4 kwa 400 mita huku miruko ni mmoja na mitupo ya kurusha mkuki,pamoja na kurusha kisahani na tufe.


Alisema dirisha la usajili lilifunguliwa rasmi tangu  juni,2022 ambapo litafungwa kwa kadri nafasi za ushiriki zinapokamilika kwa kila mchezo husika.


"Tumefanikiwa kuandikisha watoto 300 ambapo watashiriki kikamilifu katika mashindano haya ikiwa jumla ya wanariadha watakaoshiriki wametoka katika shule 50 zilizopo ndani na nje  ya jiji la Arusha ambapo wametoka mkoa wa Arusha,Manyara,Kilimanjaro na Singida,"alisema.


Zawadi mbalimbali zitatolewa kwa watoto zikiwemo medali za dhahabu,Fedha na shaba,vikombe,tuzo maalumu kwa shule na vilabu zitakazofanya vizuri pamoja na vyeti  vya ushiriki.


                        Kocha mkuu wa riadha nchini,Suleman Nyambui


                      Katibu wa chama cha riadha mkoa wa Arusha,Rogath John

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI