Na fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam
Tanzania kesho inaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku ya umoja wa mataifa duniani ambapo huadhimishwa kila ifikapo October 24 kila mwaka huu .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Nassour Mbarouk amesema kuwa mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo ni Waziri wa Katiba na Sheria Damas Ndumbaro.
Aidha amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo ambapo amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 193 ambazo zinashiriki maadhimisho hayo.
Kwa upande wake, Balozi Mratibu mkaazi kutoka UN Zlaten Milisic amesema kuwa, katika maadhimisho hayo kupitia kauli mbiu yake wanatakiwa wasimuache mtu nyuma katika masuala ya maendeleo.
Aidha, amesema anamshukuru Rais kwa mdau mzuri katika masuala ya diplomasia ambapo Tanzania imekua ikijitolea sana katika nchi nyengine kwenye kudumisha amani.
0 Comments