Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam
Serikali kupitia Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imewataka wanafunzi kutumia mitandao ya kijamii ili vizuri kuepuka kutuma ujumbe au picha zisizo na maudhui mazuri.
Kauli hiyo, imetolewa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha usalama Mtandaoni Wizara ya Habari Mawasiliano Teknolojia ya Habari Mhandisi Steven Wangwe wakati wa akitoa elimu katika shule ya wasichana Jangwani iliyopo Dar es salaam ikiwa ni mwezi wa kampeni ya kuadhimisha juu ya usalama mtandao duniani.
Amesema kuwa, usalama wa mtandaoni huanza na mtu binafsi hivyo wameanza kutoa elimu katika kundi hilo la wanafunzi mapema ili kuwa nusuru wasije wakapoteza fursa za kielimu, kiajira zilizopo mbele yao kwani kupitia mtandao watu hufuatilia mtu anachokifanya bila yeye kujua hivyo amewasisitiza kuwa makini na maudhui ya mtandaoni.
Amesema kuwa, kipindi hichi kumezuka mtindo wa watu kujipatia fedha kupitia mtandao kwa kufuatilia mtu kupitia simu yake na kuiba ikiwemo video au picha kisha kumdhalilisha kwa kutuma mtandaoni na kudai pesa ili asitume hivyo wameamua kuwapatia elimu mapema wanafunzi namna ya kuseti simu zao na kuzitumia vizuri.
Kwa upande wake, Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Jangwani, Salum Kilipamwambu ambae pia ni Mratibu Shule mtandao iliyopo chini ya Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari amesema wao wanatoa elimu lakini walimu wengi hawana elimu ya usalama wa mtandao, hivyo Serikali unatakiwa kuliangalia jambo hili katika hatua pana zaidi Ili elimu iwafikie wanafunzi wengi zaidi.
"Wanafunzi hawa pamoja na kusoma mambo ya darasani lakini wanatakiwa waielewe dunia ya Ulimwengu wa teknolojia ikoje kwani kwa sasa wanasoma kompyuta,wanatumia simu na kutumia vifaa mbalimbali vya tehama hivyo wasipojua namna ya kuvijua hasara na faida zake"amesema Mwalimu.
"Somo la teknolojia ya habari na Mwasailiano(TEHAMA) shuleni linafundishwa lakini halipewi kipaumbele katika ufundishwaji ,hivyo tunaiomba serikali itilie mkazo somo hili muhimu kwa wanafunzi ili wajue mapema matumizi sahihi ya mtandao"amesema Mwalimu Kilipamwambu.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi waliyopewa elimu juu ya matumizi usalama mitandao akiwemo Anna Ngowi ambaye anasoma kidato cha 6 shuleni hapo amesema hatua ya Wizara ya habari kutoa elimu hiyo ni yakuungwa mkono kwani imewapa elimu nzuri juu ya jinsi gani wataepuka matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.
"Kwa sisi wanafunzi tunashukuru kwa kupewa elimu hii,na tumejifunza ni vitu gani vya kuposti na visivyo vya kupost mitandaoni ili visitudhalilishe na kupelekea kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji wa kimtandao (cyber bullying)hivyo nawaomba vijana wenzangu hasa wanafunzi watumie vyema mitandao"amesema Neema Matilda ambaye ni wanafunzi wa kidato cha 5 shuleni hapo
0 Comments