Header Ads Widget

SERIKALI YATENGA MAENEO YA KUHIFADHI WAGONJWA WA EBOLA

 

Mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Dkt Sylvia Mamkwe akizungumza na vyombo

Viongozi na wadau wa sekta ya afya jiji la Arusha wakiwa katika kikao maalum cha kujadili namna ya kuchukua tahadhari endapo ugonjwa huo utaingia nchini.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Pamela Mollel,Arusha 

Serikali Mkoa Arusha imeanza mkakati maalumu wa kutenga maeneo ya kuhifadhi wagonjwa wa ebola endapo watatokea kutokana na kuripotiwa ugonjwa huo  kuwepo nchi jirani


Akizungumza katika kikao cha afya ya msingi kilichoshirikisha Viongozi na wadau wa afya jijini Arusha Mkuu wa Mkoa Arusha John Mongella amewataka wataalamu wa afya kutoa elimu kwa wananchi juu ya ugonjwa wa Ebola na namna ya kuchukua tahadhari 


Mongella alisema kuwa wananchi wakipewa elimu ya kutosha itasaidia wao kuchukua tahadhari kabla ya hatari


"Hii elimu pelekeni vijijini wananchi huko hawana uelewa juu ya uwepo wa ugonjwa wa hatarii wa Ebola "alisema Mongella 


Kwa upande Mganga Mkuu wa mkoa wa Arusha Dkt Sylvia Mamkwe alisema kuwa lengo la kikao hicho ni kujadili kwa kina namna ya kuchukua tahadhari endapo ugonjwa huo utaingia nchi


Amesema kwa sasa hakuna mgonjwa aliyeripotiwa kuwa na ugonjwa huo hatari na serikali inaendelea kuchukua hatua namna ya kukabiliana nao


Aidha mamkwe alisema jumla ya  watumishi 122 wa afya wameandaliwa kutoa elimu katika maeneo mbalimbali vijijini 


"Kwa sasa tunakabiliwa na changamoto ya vifaa ila serikali inapambana kuhakikisha inapata vifaa vya kukabiliana na ugonjwa huo"alisema Mamkwe 


Dalili za ebola ni kutoka kwa damu maeneo mbalimbali ya mwili kama vile masikioni,mdomoni,puani 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI