ALIYEWAHI kuwa Waziri wa Elimu Profesa Jumanne Magembe ameunga mkono kupunguza miaka ya elimu ya Msingi kutoka miaka saba hadi sita.
Aidha ametaka kufanyika maboresho ya elimu ya awali ili iendane na maboresho ya Elimu ya Msingi.
Maghembe aliyasema hayo Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro alipozungumza na waandishi wa habari kuwa ili kuendana na hali halisi ya sasa haipaswi wanafunzi kusoma muda mrefu.
Maghembe ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mwanga alisema kuwa elimu ya sasa inafuata misingi ya kikoloni ambapo mwanzo waliwasomesha watoto muda mrefu.
Alisema waliweka miaka mingi wawe wakubwa ili wakimaliza wawe walimu na makarani.
Alisema kuwa ili kuendana na miaka sita kuna haja ya kuhakikisha elimu ya awali inaboreshwa.
0 Comments