Header Ads Widget

PASCAL MSIGWA AWASHUKURU WAPIGAKURA -SONGEA

 

Na Amon Mtega,Matukio Daima App ,Songea.

MJUMBE wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Songea Mjini Mkoani Ruvuma Pascal Msigwa(Top One In) amewashukuru wapigakura waliomchagua kuitumikia nafasi hiyo huku akiwaahidi hatawaangusha katika uwakilishi huo.


Msigwa ambaye ameshinda ujumbe wa Halmashauri kuu Wilaya kwa kura zaidi ya 500 huku wapigakura walikuwa 748 katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa kuwapata Viongozi wa CCM watakao ongoza kwa muda wa miaka mitano.


Mjumbe huyo ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya siasa ngazi ya Wilaya baada ya kuchanguliwa tena kwa kura 81 za ujumbe wa kamati ya siasa huku wapigakura wa kuchagua Wajumbe wa kamati hiyo walikuwa 98 amesema kuwa imani waliompa wapigakura ni kubwa hivyo ataenda kufanya kazi kwa maslai ya Jamii na kuendelea kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM.



 Katika uchaguzi huo Wajumbe wamemchagua mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo kuwa ni Mwinyi Abdallah Msolomi na mwenezi ni Marco Mbawala ambao watakaoshirikiana na kamati nzima ya siasa pamoja na wanaccm wengine katika kutekeleza Ilani ya Chama hicho.

       


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI