MWAJUMA Nyamka amefanikiwa kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kibaha Mjini kwa kumwangusha aliyekuwa Mwenyekiti Maulid Bundala kwa kura 347 kwa 173.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Mjini Kibaha msimamizi wa uchaguzi Josephine Mwanga alimtangaza Nyamka kumshinda Bundala ambaye alikuwa mwenyekiti kwa kipindi cha miaka 15.
Mwanga alimtangaza aliyekuwa katibu wa CCM Mkoa wa Pwani Sauda Mpambalyoto aliyepata kura 33 na mshindi wa nne alikuwa ni Abdala Mdimu ambaye naye aliwahi kuwa katibu wa CCM Kibaha Mjini aliyepata kura 32.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uchaguzi huo Nyamka alisema kuwa anawashukuru wajumbe na kutaka makundi yote yavunjwe libaki kundi moja la CCM.
Nyamka alisema kuwa kiluchobaki ni kukijenga chama ili kiwatumikie wananchi kwa kuwaletea maendeleo na kudumisha upendo na mshikamano.
Naye Maulid Bundala alisema kuwa anawashukuru wajumbe kwa kumwamini kwa kipindi chote alichokiongoza chama na atashirikiana na mwenyekiti huyo kukipambania chama.






0 Comments