Ndege ya kijeshi imeanguka katika eneo la makazi ya watu katika mji wa Yeysk kusini mwa Urusi.
Picha ambazo hazijathibitishwa za tukio hilo zilionyesha moto mkubwa ukiteketeza jengo kubwa la ghorofa .
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema ndege hiyo aina ya Su-34, ilikuwa kwenye safari ya mafunzo wakati injini yake moja iliposhika moto.
Bado hakuna habari kuhusu majeruhi, lakini ambulensi na vyombo vya moto vilionekana kwenye eneo la tukio.






0 Comments