Header Ads Widget

MRADI WA KILI SES WAKUTANISHA WANAFUNZI MBALI MBALI DUNIANI MKOANI KILIMANJARO

 


MRADI wa KILI SES umewakutanisha wanafunzi mbalimbali dunian Mkoani Kilimanjaro lengo ni kufanya utafiti wa mazingira katika maeneo yanayozunguka mlima  Kilimanjaro.


Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Kilimanjaro Meneja wa mradi huo Claudia Hemp amesema kuwa wanafanya utafiti wa aina mbalimbali ili kuangalia ni namna gani wataaweza kuboresha mazingira .


Ameyasema kuwa wanafanya utafiti kuangalia ni jinsi gani watu wanaweza kuishi bila kufanya uharibifu wa mazingira.




Anjela Nyaki akizungumzia mradi huo amesema mraadi huo utakuwa na vitu vingi ambavyo vitasaidia kutunga sera ya juu ya uhifadi wa msitu wa mlima Kilimanjaro na kuleta manufaa kwa wananchi.


"Wananchi wanashirikishwa kwenye vitu vingi Kama wale wanaofanya utafiti wa maji na udongo ndani ya hifadhi na nje ya hifadhi "


"lla Mimi kwa upande wangu nitafanya upande wa magharibi wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro na nitaangalia zaidi ekolojia ya upande ulle hasa kwenye Ile korido ya kitendem ambayo inaunganisha hifadhi ya mlima Kilimanjaro na maeneo ya mtawanyiko wa sihaa pamoja na hifadhi ya jamii endumert pamoja na kule upande wa kenya kwenye hifadhi ya embosenyi ambapo wanyama wanatoka Kilimanjaro na kushuka mpaka kule Amboseri "Alisema Nyaki.


Sambamba na hayo amesema kuwa ataongea na jamii ya kule na kutumia camera traps lengo ni kujua ni aina gani ya wanyama wanatoka mlima Kilimanjaro na kwenda katikaa hifadhi ya emboseri.



Kwa upande wa wa wanafunzi walioshiriki akiwemo Neema Robart Kinabo  Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamifu kupitia mradi wa Kili Ses amesema kuwa mradi huo ni muhimu sana kwani itaasaidia kuangalia Mahitaji ya kibinadamu , mazingira na namna mazingira yanavyoathiriwa na matumizi mbalimbali ya ardhi pamoja na mabadiliko ya Tabia ya Nchi.


Hata hivyo ameishauri jamii kuitunza mazingira ya asili yanayowazunguka kwani wasipoyatunza yatapelekea ukosefu wa mahitaji mbalimbali yanayotokana na Mazingira.


John Julius Mwanafunzi wa PHD  amesema kuwa katika utafiti wa awali Umeonesha kuwa wazee wa zamani walikuwa wanatumia maarifa katika kutunza mazingira ya zamani.


"Inaonekana kwa sasa vijana wengi wamekuwa wakidharau maarifa hayo na kuona kwamba imepitwa na wakati na ndio maana wengine wanaamua kutoka vijijini na kwenda Kuishi mjini kwa hiyo Sasa wanapoondoka kwenda mjini wale wazee wanakosa watu wa kuwapa Yale maarifa "Alisema.


Nao wadau wa mazingira walioshiriki katika mkutano huo akiwemo mchungaji wa Kanisa la kiinjili la kilitheri Tanzania (KKKT) Faustina Mmary amesema kuwa ni wajibu wa Kila mtu kutunza mazingira.


"Kwanza kabisa Mungu alivyotumba kazi ya kwanza aliyotupa ni kutunza bustani ya Edeni tuitunze na tuilime ndio kazi ya kwanza tuliyopewa na alitupa wanyama tuwaite majina Kama maandiko yanavyosema"






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI