Header Ads Widget

MAONESHO YA WIKI YA CHAKULA DUNIANI KUFANYIKA SIMIYU

 

Na Zulfa Alphan,Matukio Daima App Simiyu 

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda amesema mkoa huo unatarajiwa  kuwa mwenyeji wiki ya chakula duniani itakayofanyika oktoba 10 hadi 16 ,2022.


" Mkoa wetu wa Simiyu umepewa heshima kubwa ya kitaifa ya kuwa wenyeji wa maadhimisho ya siku ya chakula duniani 2022"


Dkt Nawanda amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuhamasisha uzalishaji na upatikanaji wa chakula bora, salama na cha kutosha kuanzia ngazi ya kaya, wilaya , mkoa na taifa kwa ujumla huku yakienda sambamba na maagizo ya mhe, Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwata wakuu wa mikoa kuhakikisha wanaboresha lishe katika kaya za mikoa yao.


" Kwahiyo mhe, Rais ametutaka wakuu wa mikoa na wakuu wote  wilaya kuhamasisha wananchi wanapata lishe bora katika ngazi ya kaya ili kuongeza ufanisi...kupunguza udumavu katika kaya zetu " amesema Dkt Nawanda 


Amesema katika kufanikisha maandalizi ya maonesho hayo mkoani hapo wataenda kushirikiana na wizara za  kilimo , mifugo na uvuvi ,wizara ya afya na washirika  wa maendeleo  wakiongozwa na shirika la chakula na kilimo  duniani ( FAO) .  

  

Maadhimisho hayo yataambatana na utoaji wa elimu ikiwemo maonesho ya teknolojia mbalimbali za uzalishaji usindikaji ,uhifadhi , uandaaji wa chakula, ulaji bora kwa afya bora pamoja na huduma zingine zinazotolewa na wadau na taasisi mbalimbali katika mnyororo wa thamani.


" Ni eneo moja ambalo tunaenda kuwaonesha wananchi sisi watu wa Simiyu tunalima nini na tunazalisha nini lakini pia tunakula nini kwahiyo ni fursa moja wapo kuja kuona chakula cha wananzengo wa Simiyu tunakula nini ..matobolwa ,choroko, dengu ,ugali mwekundu , uwele ...lakini pia tutakuwa na shughuli mbalimbali kwa mfano kupeleka sahani yenye chakula cha mlo kamili katika hifadhi ya wanyama Serengeti ili kuhamasisha ulaji wa mlo kamili...lakini tutaendelea  kuhamasisha matumizi ya  ulaji wa vyakula vya asili ...maharage choroko dengu nk "amesema Dkt Nawanda na kuongeza kuwa: 


" Wapikaji wakubwa wale nguli pia tutawapa nafasi ya kuonesha unguli wao ili waweze kupeleka taarifa/ elimu kwa dada zetu ...mabinti zetu waone sasa akina bibi zetu zamani walikuwa wanapika nini na leo hii wao wanapika nini ili waendeleze kuboresha..tutashindanisha wanafunzi katika vipaji mbalimbali ikiwemo uchoraji wa mambo yanayohusiana na ule mnyororo wa mzima wa lishe ..kuwaandaa wanafunzi katika nyimbo mbalimbali ikiwemo mashairi na ngojere katika kuhamasisha ujumbe wa mwaka huu " amesema Dkt Nawanda .


Maonesho hayo yanaenda sambamba na kauli mbiu isemayo" ni uzalishaji bora ,lishe bora, mazingira bora kwa wote abaki mtu nyuma " huku mgeni  akitarajiwa kuwa waziri wa kilimo Hussein Bashe.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI