Header Ads Widget

KILIMO CHA VANILA NI DHAHABU YA KIJANI

Na Thabit Madai,Zanzibar – MATUKIO DAIMA

SERIKALI na Wananchi kwa Ujumla wametakiwa kuweka Mikakati Imara katika kuinua kilimo cha Vanila ambacho kinatajwa kuwa Mkombozi  wa Uchumi wa Zanzibar badala ya Wananchi kutegemea mazao ambayo yamekuwa yakilimwa kwa mazoea lakini bila kuwanufaisha Wakulima.

 

Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi mte daji wa Vanila International Simon Mkodya wakati akizungumza na Waandishi wa mbalimbali wa Habari Nchini ambapo amesema ni vyema kwa Serikali na Wananchi kuwa na Mkakati imara katika kushirikia kulima zao la Vanila ambalo lina tija kwa Uchumi wa Zanzibar.

 


Amesema Kilimo cha Vanila kwa sasa kina tija kubwa ukilinganisha mazao mengine hivyo ni vyema kilimo hicho kikawa kipaumbele cha Serikali na Wananchi.

 

“Nataka kuwaambia Wananachi na Serikali kwamba katika ile Orodha ya Mazao Mkakati wanatakiwa kuliweka zao la Vanila kama zao namba moja kutokana na kuwa na tija kubwa,” ameeleza.

 

“Kilo Moja ya Vanila katika Soko la Dunia inafika hadi milioni Moja na Nusu hivyo zao hili lina tija ukilinganisha na Mazao mengine hivyo nawaambia Wananchi na Serikali kuweka zao hili katika orodha ya mazao ya mkakati ili kuinua uchumi wa Nchi,”amesema.

 

Akizungumzia Mradi huo wa Kilimo cha Vanila amesema kwamba Kilimo hicho wanakiendesha katika eneo la lenye ukubwa wa Herkali zaidi ya 60 na Kuwashirikisha Vijana mbalimbali ndan ya Visiwa vya Zanzibar.

 

“Hadi sasa Kilimo hichi kimewanufaisha Vijana mbalimbali kutokana kuwa ndani ya Kilimo cha Vanila kuna mazao mengine ya Biashara yanazalishwa katika eneo hili, ameelezea.

 

Nae Ashura Masoud Makame ambae ni Mkulima ameelezea namna ambavyo kilimo hicho kinavyowanufaisha wao kwa kupata ajira na kuingiza kipato ambacho kinaendesha maisha yao.

 


“Kwa sasa tunafaidika kwa kupata ajira na kuingiza kipato cha Uhakika kutokana na uwendeshaji wa Kilimo cha Vanila katika eneo la Bungi,” ameeleza.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI