YAHAYA Mtonda amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kibaha Mjini baada ya kupata ushindi kwa kujinyakulia kura 159.
Msimamizi wa uchaguzi huo uliofanyika picha ya Ndege Kibaha Aishe Rajabu alimtangaza mshindi wa pili kuwa Simon Luhende aliyepata kura 81 akifuatiwa na Mariaconsolata aliyepata kura 63.
Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo Mtonda alisema kuwa ataifanya Jumuiya hiyo kuwa na vyanzo vyake vya mapato ili ijiendeshe na kutokuwa tegemezi.
Mtonda alisema kuwa ataanzisha vikundi vya ujasiriamali na atavitafutia vikundi hivyo taasisi za fedha ili vipate mikopo ikiwa ni pamoja na ile inayotolewa na Halmashauri kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao za kiuchumi.
Tully alisema kuwa viongozi wote waliogombea walikuwa bora Ila wanachama wametimiza wajibu wao kuchagua viongozi wanaowahitaji.
Alieleza kuwa anaimani na viongozi waliochaguliwa watakwenda kuivusha Jumuiya na kuwataka kuwa wamoja kusimamia ili ipige hatua za kimaendeleo.






0 Comments