Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
KATIBU Mtendaji Bodi ya filamu Tanzania Dkt,Kiagho Kilonzo amesema Bodi hiyo inaratibu Kamati Maalum ya kutetea haki za Wasanii iliyoundwa na Waziri mwenye dhamana Mohamed Mchengerwa lengo likiwa ni kusimamia masuala ya Sanaa nchini na upatikanaji wa haki kwa wasanii.
Akiongea na waandishi wa Habaari leo October 4 Jijini Dodoma Wakati akieleza utekekezaji wa majukumu ya Bodi ya Filamu Katibu Mtendaji huyo alisema hadi sasa kamati imeshapokea malalamiko 30 na kuyashughulikia, ambapo takriban shilingi milioni 300 zilizokuwa zimedhulumiwa zimesharejeshwa kwa wasanii.
Aidha alisema Malalamiko 22 yamesuluhishwa, na Malalamiko 8 yapo katika hatua mbalimbali za kushughulikiwa.
"Baadhi ya malalamiko yaliyopokelewa na kushughulikiwa ni yale ya marehemu Amri Athumani (King Majuto), marehemu Steven Kanumba, msani David Ganzi (Young Dee), Mzalishaji wa Tamthilya Samwel Isike, nk ," Alisema Katibu Mtendaji huyo.
Kuhusu Masoko na Usambazaji wa Filamu
Alibainisha Kuwa Serikali imeendelea kuwekewa mazingira wezeshi kwa wadau wa Filamu kujiajiri, hivyo kuongeza na kukuza pato la Taifa, kupunguza umaskini na kuchochea maendeleo ya Sekta nyingine mtambuka kama vile Utalii.
Baadhi ya miundombinu iliyopo na iliyoanzishwa ni usambazaji kupitia Vituo vya Televisheni za hapa nchini zinazoonyesha Saa 24 Siku 7 za Juma pamoja na mifumo ya kidijitali inayoonyesha filamu za kitanzania nyingine ni kumbi tisa (9) za kisasa za Sinema [Dar (Kumbi 4), Arusha (Kumbi 2), (Ukumbi 1), Mwanza (Ukumbi 1) na Dodoma (Ukumbi 1)].
Alieleza Bodi imeunda Kamati maalum ya kurudisha utamaduni wa kutazama filamu katika Kumbi za Sinema hatua hiyo inatarajiwa pia kutoa mchango stahiki katika uchumi wa wadau wa Sekta na Taifa kupitia viingilio vya mlangoni.
Kwa upande wa usambazaji Serikali ina makubaliano na kimataifa Televisheni Mtando ya Nuella (Nuella Online TV) ya nchini Uholanzi kununua na kuonesha Filamu za Kitanzania, na hadi sasa kuna filamu tisa (9) zinaonyeshwa huko.
Fursa za Ajira
Alisema kwa kipindi cha Januari hadi Disemba, 2021 pekee inakadiriwa kuwa ilichangia takriban ajira 30,000 zilizotokana na Filamu (waigizaji, waandaaji na watoa huduma).
Kwa mazingira ya Kitanzania, Filamu moja (wastani wa watu 20, tamthilia moja wastani wa watu 100).
Kiasi hicho ni ongezeko la nafasi 5,000 kutoka 25,000 kiasi kinachokadiriwa kuzalishwa mwaka 2020.
Kwa Upande wake Msemaji mkuu wa Serikali Gerson Msigwa alisema Bodi ya Filamu ni Kati ya nyenzo inayotumika katika kutangaza nchi kwa kupitia Filamu za wasanii hivyo basi Wasanii hawana budi kutembea kifua mbele kwani sanaa ndio kitu kinachoitangaza nchi .
" Kuipitia sana nchi yetu itakwenda kujulikana hivyo basi kupitia sanaa zetu Sasa tukaitanagaze nchi yetu kwa vivutio tulivyonavyo twende tukaitangazie dunia madini yetu na hata vyakula vyetu vya kitanzania" Alisema Msingwa
Mwisho.







0 Comments