Mkuu wa Kanisa la kiinjili la kilitheri Tanzania KKKT Askofu Fredrick Shoo amesema kuwa chuo Cha theologia na biblia mweka ni chuo Bora kinachotoa wanafunzi wanaofanya kazi kwa uledi na kuwa na nidhamu pindi wakiwa makazini.
Askofu Shoo amesema hayo wakati alipokuwa katika Mahafali ya 64 ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Pia ameipongeza chuo hicho kwa kuwaandaa watumishi wazuri wa Kanisa wa kada mbalimbali wanaoenda kufanya kazi katika Shamba la bwana .
"Mkuu wa chuo chuo na wakufunzi wa chuo hichi Cha mwika limekuwa ni chuo Cha kipekee sana katika historia ya Kuandaa watumishi wa Kanisa Hilo la kiinjili la kilitheri Tanzania lakini pia hata nje ya nchi yetu na kwa namna hiyo chuo hiki limekuwa baraka kwa Kanisa kimekuwa baraka kwa watu wa Mungu na sehemu nyingine"Alisema Shoo.
Sambamba na hayo amesema kuwa chuo hicho kimetoa elimu na taaluma pamoja na kuwaandaa watumishi ambao wameandaliwa kimaadili na kwamba wanahitimu wakiwa mfano katika maeneo wanayoenda kufanya kazi ya bwana.
"Na hapa Mkuu wa chuo nakuambia wanafunzi wameonesha tofauti kubwa sana na watumishi wanahitimu katika vyuo vingine katika taabia ,mwenendo na Utumishi wao ,na Mimi ninapenda kuwaomba muendelee hivyo hivyo kutuzalishia watumishi wa aina hiyo hiyo "Alisema Dr.Shoo.
Sambamba na hayo amewataka wahitimu waliohitimu katika chuo hicho kuingia katika huduma hiyo ambayo bwana Yesu mwenyewe aliwaitia na kulishika neno ambayo ni kauli mbiu Cha chuo linalosema neno la msalaba ni nguvu yetu .
Amesema kuwa ni vyema wakapeleka neno la Mungu kwa kusema kuwa Dunia Bado inamhitaji Yesu ,inahitaji neno la msalaba na kueleza kilichofanyika pale msalabani kwa ajili ya ukombozi wetu.
Naomba mkawe wajumbe wa Yesu kristo na kazi zake nawaombeni saana ili muweze kuwa watumishi wema wa Yesu kristo tafadhali muende na muwapende wale mtakaopewa kuwahidumia kwani pasipo Upendo huduma yenu itakuwa ya manunguniko ,mkawahudumie watu wa Yesu kristo kwa bidii zote Kama wafuasi wa kweli wa Yesu kristo na hili napenda kuomba tu kwamba wakati wote ujikumbushe kwamba wewe ni mtumishi wa Yesu kristo.
Hata hivyo amewataka wanafunzi hao kutoenda kufanya mambo ya kisanii Kama yanavyoonekana kwa watu wanaojiita watumishi na kuomba kwa kusema katika miaka yote waliyosoma japo chuoni hawajaandaliwa kuwa wasanii Bali wameandali kwa ajili ya kuihibiri injili.
Kwa upande wake makamu Mkuu wa chuo hicho John Materu akisoma historia ya chuo hicho amesema kuwa chuo hicho kilianzishwa mwaka 1953 na Kanisa la kiinjili la kilitheri Tanganyika ya Kaskazini ambapo kwa sasa chuo hicho kipo chini ya uongozi wa Kanisa la kiinjili la kilitheri Tanzania dayosisi ya Kaskazini.
Amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa chuo hicho ni kuongoza kozo fupi fupi kwa wakristo raiya kwa nia ya kuwajengea Msingi imara wa ufahamu wa neno la Mungu na Imani ya kikristo na baada ya kozi hizo waliweza kutumika katika Kanisa Kama wazee wa Kanisa ,waalimu wa shule ya jumapili na waalimu wa shule za biblia sharikani.
"Kwa sasa Bado chuo kinaendeleza utaratibu huo wa kuwa na kozi fupi fupi hasa wakati wa likizo ndefu "
Amesema kuwa kusudi la pili ni kwaandaa watumishi wa Kanisa kwa wakati ule wainjilisti,wasadizi wa huduma za jamii,wanamiziki wa Kanisa na baadae wachungaji.
Amesema kuwa changamoto zinazowakabili chuo hicho ni pamoja na msongamano uliokithiri katika bweni la Wanawake kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi Wanawake ukilinganisha na miundombinu ya chuo hicho na Kama inavyoonekana idadi ya skina mama inaongezeka siku Hadi siku .
Changamoto nyingine ni athari za ukame unaoathiri upatikanaji wa chakula Cha kutosha kwa wanachuo ,pamoja na ukosefu wa mtandao wa kuaminika na kujitosheleza katika matumizi ya chuo kizima ,
Amesema kuwa chuo kina mpango wa kupanua bweni la wanafunzi wanawakewa kwani idadi ni kubwa tofauti na ilivyokusudiwa awali, na kuimarisha kitengo Cha utafiti kwa lengo la kukabiliana na changamoto zonazoibuka katika Kanisa kwa wakati huu.
Hata hivyo mahafaali hayo yaliambatana na uzinduzi wa bwalo la chakula na jiko lalilogharimu zaidi ya milioni mia sita sita na ambapo Ujenzi huo ulianza tarehe 23-,6 -2017 huku wakishirikiana na wageni kutoka nje ya nchi.
Akihubiri neno la Mungu katika Mahafali hayo Mkuu wa Kanisa la kiinjili Bavaria lililop ujerumani Dr.Strohn Bedford Heinrich amewambia wanafunzi hao kwamba kwa masomo waliyopata chuoni hapo inaonesha ni jinsi gani wameandaliwa kwa ajili ya kwenda kuihibiri injili kwa watu wote.
0 Comments