NA WILLIUM PAUL, SAME.
Mashindano hayo yatakayokuwa yakishindanisha timu za tarafa yalishudiwa yakianza jana katika Tarafa ya Mamba vunta ambapo timu 20 zinashiriki mashindano hayo.
Kwa mujibu wa Mbunge wa Jimbo la Same mashariki, Anne Kilango Malecela ambaye ndio mfadhili wa mashindano hayo amedai mshindi wa kwanza Hadi wa tatu wataondoka na zawadi nono ambayo haijawahi kutokea.
"Mashindano haya kwa Tarafa ya Mamba vunta yatakuwa ya siku 10 na zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu haijawai kutokea katika Jimbo lolote hapa nchini itakuwa zawadi nono ili kuwapa motisha vijana wangu wa Jimbo la Same mashariki" alisema Anne Kilango.
Mbunge huyo alisema kuwa, lengo la kujikita katika michezo ni kuhakikisha anainua vipaji vya vijana huku akidai kuwa kwa sasa michezo ni fursa ya ajira na kuzitaka timu zinazoshiriki katika ligi kuu pamoja na ligi za chini kufika kujionea vipaji.










0 Comments