Na Matukio DaimaAPP Iringa
KATA ya Ilala ni moja kati ya Kata 18, zilizopo katika manispaa ya Iringa, ni kata iliyobeba chuo kikuu bora na mashuhuri chuo cha Mkwawa tawi la Mlimani University (UDSM).
Asilimia 95 ya ilani ya chama cha mapinduzi iliyoahidiwa imetekelezwa vyema ndani ya mipaka yote ya Kata ya Ilala.
Maendeleo yakiwemo, miradi mbalimbali, miundombinu, vikundi vya vijana na akina mama, elimu na michezo imefanya wananchi wa Ilala kuamini Kwa macho kwamba chama cha mapinduzi kinatekeleza Kwa vitendo ilani yake ndani ya Ilala.
Conrad Mlowe ni mheshimiwa diwani anayeperurusha bendera ya chama cha mapinduzi kwenye kata hiyo,Mlowe anahakikisha ahadi zote zilizoahidiwa 2020 kwenye kampeni zinatekelezwa kwa wakati.
Kwa upande wa elimu na michezo, Mh Conrad Mlowe amejitahidi kuelimisha vijana wa kata ya Ilala namna bora ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya ukimwi pamoja na kuto kukaa vijiweni bila kazi, kwa kuanzisha michezo na kuwapatia vifaa vya michezo ikiwemo mipira pamoja na jezi kwa timu zote zilizo ndani ya kata ya Ilala.
Kwa upande wa miundombinu, Mh Mlowe amejitahidi kuweka mazingira bora na salama ya barabara pamoja na mifereji iliyokuwa kero na adha kubwa kwa wananchi wa mitaa ya Ilala mfano hapo awali kipindi cha. mvua wananchi wa mitaa wa kijificheni kuanzia maeneo ya Mlamke sekondari hadi Mchambawima walilalama na kupata adha kubwa kwa kuingiliwa na maji taka pamoja uchafu uliosombwa na maji hadi kwenye makazi yao.
Kwa kuliona hilo Mh Mlowe pamoja na wadau mbalimbali wameweza kutengeneza mtaro madhubuti na imara, utakao wafanya wananchi wa mitaa hiyo kuto kupata kero tena ya maji taka na uchaafu katika makazi yao.
Kwa upande wa vikundi vya ujasiriamali Mh Mlowe yupo mstari wa mbele kuwahamasisha vijana waendelee kujiunga na vikundi mbalimbali ili waendelee kufaidi fedha zilizo tengwa kwaajili ya vikundi huko halmashauri, Mh Mlowe amemaliza kwa kusema ifikapo 2025 asilimia 88 ya vijana na akina mama watakuwa wamepata mikopo pamoja na ajira huku wafanya biashara wakitengenezewa mazingira mazuri katika kazi zao, Mlowe amewasihi wananchi waendelee kumuunha mkono Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan kwani ana mengi mema juu ya nchi ya Tanzania pamoja na kata ya Ilala.







0 Comments