NA TITUS MWOMBEKI, Matukio Daima App Kagera.
BAADHI ya watu wenye ulemavu mkoani kagera wameziomba halmashauri zote nchi kuweka utaratibu mzuri utakaosaidia kuwandolea changamoto wanapokwenda kuomba mikopo inayotolewa na halmashauri hizo kwaajiri ya kujikwamua kimaisha.
Hayo yamesema na Christiani Kabuka mkazi wa Kata ya Rwamishenyi inayopatikana katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ambaye ni mlemavuwa wa viungo katika mahojiano maalumu nachombo hiki ambapo amesema kuwa baadhi ya watu wenye ulemavu amekuwa wakishindwa kwenda kuchukua ya 2% iliyotenga na halmashauri kwa watu wenyeulemavu kutokana na mrolongo mrefu mpaka kupata mikopo hiyo.
“Tunashukuru serikali kupitia halmashauri kwa kututengea 2% ili na sisi tuweze kujikwamua kiuchumi lakini pia bado kuna changomoto ndogo ndogo ambazo halmashauri zetu zinatakiwa kuzianagalia, sisi ni watu wenye ulemavu unakuta unapokwenda kuchukua mkopo wasituzungushe watufanyie wepesi unakuta unaambiwa rudi kesho rudi leo ukiangalia na hali zetu wengine tunatoka mbali hili jambo linapelekea baadhi ya wanavikundi kukata tama”
Naye Sweetbert Mushanga Katibu wa shirikisho ya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA) Kagera ameipongeza serikali na halmashauri zote kwa kutenga 2% kwaajiri ya watu wenye ulemavu ili nao waweze kujikwamua kiuchumi huku akishauri kuwa kutokana na hali zao halmashauri zinatakiwa kuweka utaratibu wa kuwa inawaita watu wenye ulemavu mara kwa mara na kuwapatia semina pamoja na mahitaji yote yanatakiwa hili mtu mwenye ulemavu aweze kupatiwa mkopo.
“Unakuta baadhiya watu wenye ulemavu wengine wanakuja kuomba mikopo huku awajuhi ni mambo gani yanahitajika ili wao waweze kupatiwa mikopo hiyo hiyo mimi nashauri halmashauri iandae utaratibu wa kuwa inawaita mara kwa mara na kuwa elimisha vitu gani vinatakiwa na mahitaji hayo nasio kwa maneno bali yawekwe kwa njia ya maandishi ili kuondoa changamoto nenda rudi ukamilishe hiki”
Kwaupande wake Afisa Maendeleo ya Jamii katika Manispaa ya Bukoba,Murshid Issa amesema kuwa ili kundokana na changamoto hiyo serikali kupitia halmashauri pia ilianzisha mfumo maalumu wa kuomba mikopo kwa njia mtandao kwa vikundi vyote likiwemo kundi la watuwenye ulemavu unaojulikana kama MIKOPO YA 10% YA HALMASHAURI ili kusaidia kurahisisha uombaji wa mikopo hiyo kwani kila kitu kinachohitaji mfumo uwaelekeza.
“kinachohitajika ni mtu kuingia kwenye unahitwa TPL Mis na kuanza kujaza taarifa zote za kikundi, mfumo huu ni mzuri kwani unamuelekeza kila kitukinacho hitajika na anaweza kuomba popote pale anapokuwa sisi huku tunapatiwa taarifa na akikamilisha anakuja kuchua”
Ameongeza kuwa nje na kupunguza changamoto ya nenda rudi mgumo huo unazisaidia halmashauri kutatua changamoto ya watu kuomba mikopo zaidi ya kikundi kimoja kwani kupitia mfumo huo inahitajika nambaya NIDA ambayo ina taarifa zote za muombaji wa kopo huo,huku akiwasisitiza watu wenye ulemavu kuendelea kuchangamkia fursa ya uombaji wa mkopo 2% mbili iliyotengwa kwa ajiri yao.
0 Comments