Header Ads Widget

WANAOSHIRIKI MICHEZO YA MAJESHI SARPCCO WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA, WAONYWA KUTUMIA RUSHWA

 


Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amewataka askari Polisi wanaoshiriki michezo ya Shirikisho la Jumuiya ya Majeshi ya Polisi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO GAMES) kuzingatia taratibu zote na kanuni za michezo ikiwemo kujiepusha na vitendo ambavyo havikubaliki kimichezo.


Wito huo ameutoa jijini Dar es Salaam wakati akifungua rasmi michezo hiyo katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam, huku pia akiwataka askari kujiepusha na rushwa, kupanga matokeo ya kimichezo na kuwataka kujenga uhusiano utakao saidia kudhibiti uhalifu unaovuka mipaka, usafirishaji wa binadamu sambamba na uhalifu mwingine.


"Nimesisitiza Mashindano haya yafate misingi a kanuni ambazo wamewekeana wenyewe ambapo zinakataza vitendo ambavyo havina maadili na matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu, kupanga matokeo pamoja na rushwa "amesema Masauni.


Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Camilius Wambura amesema kuwa, takribani nchi nane zinazoshiriki mashindano hayo ambayo yanawakutanisha askari na maofisa kwa pamoja na kuweza kuwa karibu na kufahamiana, na kufanya kazi kwa pamoja na kubadilishana taarifa mbalimbali za uhalifu na kiintelijensia.


 Nchi zitazoshiriki Mashindano hayo ni  Tanzania ambao ndio wenyeweji wa Mashindano hayo, Namibia, DRC, Mozambiq, Zambia, Eswatin .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI