Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amewataka wakurugenzi wa Mabonde ya maji kote nchini kuhakikisha wanasimamia na kulinda vyanzo vya maji ili visiharibiwe na wananchi
Aliyasema hayo Jijini hapa wakati akizindua Program ya sekta ya maji awamu ya tatu (WSDP III) huku akisema wananchi wamekuwa wakifanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo hivyo vya maji na yote ni kutokana na jamii kutokuwa na elimu juu ya umuhimu wa kulinda na kutunza vyanzo hivyo.
Kutokana na hayo aliwataka watendaji wote wa Wizara ya Maji kutoleta taharuki kwa wananchi wanaolima katika vyanzo vya maji kwa kufyema mazao yao waliolima na badala yake amewataka watendaji hao kutoa elimu juu ya kulinda vyanzo hivyo.
Alisema kwa sasa hali imebadilika tofauti na zamani huko nyuma kwani zamani watu walikuwa wakioga katika mito na mwabwa lakini sasa hivi hakuna vyote ni kutokana na kuharibu vyanzo vya maji.
"Naomba tusifikie hali iliyowapata wananchi wa Dar es salaam wanavyopata shida juu ya upatikanaji wa maji baada ya kuharibu vyanzo vya maji tumeshuhudia Mto Ruvu ulivyokauka maji na kupelekea Jiji hilo Kuwa na uhaba Mkubwa wa maji,"Alisema Aweso.
Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Anthony Sanga alisema wanatarajia kongamano kubwa kukutana na wadau kujadili Masuala mazima ya maji
Awali wakizungumza kuhusu mchango wa sekta ya maji Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dkt James Mdoe amesema kupitia mradi huo watajenga vyoo bora na mabomba ya kunawia mikono katika shule za msingi 2800, sekondari 1400 na vyuo vikuu.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya kilimo, mifugo na maji (Mbunge) Christina Ishengoma amesema licha yakuendelea kusogeza huduma ya maji safi na salama kwa wananchi lakini jitihada zaidi zinahitajika sambamba nakuboresha utoaji bill za maji nakusikiliza malalamiko ya wananchi.
"Tunapoboresha na kusogeza huduma ya Maji kwa wananchi tujitahidi kutatua na haya malalamiko ya kuongezewa bill za maji hii imekuwa ni changamoto wananchi wanalalamika sana"amesema Ishengoma.
0 Comments