Na Fadhili Abdallah,Matukio DaimaAPP Kigoma
WAJASILIAMALI wanawake 100 mkoani Kigoma wamepatiwa mafunzo ya kuboresha viwango vya biashara wanazozalisha kutoka Chama cha wafabiashara wanawake Tanzania (TWCC) ili kuwezesha bidhaa zao kupenya soko la Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC, Mwajuma Hamza alisema kuwa chama hicho kitaendesha mafunzo ya siku mbili kwa wanawake hao wajasilimali kutoka wilaya sita za mkoa Kigoma kuweza kuzingatia taratibu za biashara za kimataifa ili bidhaa zao zikidhi vigezo katika kutafuta masoko ya nje.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa wajasiliamali wengi wa mkoa Kigoma wanazalisha bidhaa nzuri lakini zipo taratibu ambazo zinafanya bidhaa zao zisikidhi vigezo ikiwemo suala lamazima yanayohusu biashara za kuvuka mpaka.
“Mambo hayo ni muhimu kumfanya mjasiliamali huyo mwanamke kuweka kupata soko la uhakika ambalo linahitaji bidhaa nyingi na zenye viwango bora na ili kufika huko lazima uwe na vigezo vya kukopesheka na ndiyo maana tumewaita hapa ili tuweze kuwapa mafunzo waweze kutekeleza hayo watakayofundishwa,”Alisema Mkurugenzi wa TWCC.
Alisema kuwa mafunzo hayo yanatolewa mkoani Kigoma lakini ni muendelezo wa mafunzo ambayo yametolewa kwenye mikoa mingine nchini na nchi nyingine sita za Afrika Mashariki kwa ufadhili wa shirika la Trade Mark East Afrika (MEA) ili bidhaa zinazozalishwa ziwe na ubora unaolingana kwa nchi zote za Afrika Mashariki.
Akifungua Mafunzo hayo Afrika Biashara ofisi ya Mkuu wa mkoa Kigoma,Deogratius Sangu alisema kuwa kuzingatia ubora unaosimamiwa na mamlaka mbalimbali za biashara ndiyo njia pekee itakayowafanya wajasilimali kupata mafanikio kwenye shughuli zao.
Sangu alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwani yanatoa mwongozo kwa wajasiliamali nini wanatakiwa kufanya ili biashara zawe zikubalike kwenye nchi nyingine baada ya kuwa zimethibitishwa na mamlaka za hapa Tanzania.
Pamoja na hilo Sangu alisema kuwa kuzingatia ubora kuna maana kubwa kwa taasisi za fedha kutoa mikopo kwa wajasilimali kwani wanauhakika biashara inayofanyika haitakuwa na tatizo na mamlaka zinazosimamia biashara.
Swaumu Ahamad kutoka wilaya ya Kibondo ambaye anauza bidhaa za chakula na nje ya nje alisema kuwa mafunzo kwa wajasilimali ni nyenzo muhimu katika kuzingatia mahitaji mbalimbali ikiwemo suala la vifungushio, kuwa na nenmbo ya ubora, kuwa na jina la biashara na namba ya utambulisho wa biashara vitu ambavyo vinawezesha biashara kukidhi vigezo vya kuvuka mpaka.
0 Comments