Header Ads Widget

WAGOMBEA WALIYOTUMIA KIVULI CHA SEKONDARI YA MKINGA MBINGA WASHINDA.

 



Na Amon Mtega,_Mbinga


UONGOZI mpya wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma umejipanga kuendelea kuimarisha miradi ya Jumuiya hiyo ikiwemo Shule ya Sekondari Mkinga ili kuifanya kuwa mfano kwenye Chama cha Mapinduzi CCM.


Wachaguliwa hao ambao walisimama kwa Wajumbe kuomba kura kwa kuitaja Shule ya Sekondari Mkinga inayomilikiwa na Jumuiya hiyo kuwa itazidi kuboreshwa zaidi ili kuendelea kuwawekea  mazingira bora ya wanafunzi ya kujisomea  na kuongeza ufaulu zaidi,jambo ambalo liliwavutia wapigakura na kuamua kuwachagua.




Katika uchaguzi huo Jumuiya hiyo imepata uongozi mpya huo ambapo mwenyekiti ni Hajiri Kapinga alipata kura 401 aliyemfuatia Deo Malepa alipata kura 66 na Mariether Mponda amepata kura tisa ambaye awali alijitangaza kujitoa na kumuunga mkono aliyeshinda huku wapiga kura walikuwa 602.


Kwa upande wake mwenyekiti Hajiri Kapinga wakati akiwashukuru wapigakura amesema kuwa atahakikisha anapita kwenye kata zote kubaini changamoto zinazoikabili Jumuiya hiyo kisha kuzitatua kwa pamoja.



 Mwenyekiti huyo amesema kuwa kufuatia unyeti wa Jumuiya hiyo licha ya kusimamia miradi mbalimbali ya Jumuiya lakini bado atajitahidi kupita kutoa Elimu ya utunzaji wa mazingira ili kupunguza tatizo la uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia Nchi.


Aidha Wajumbe toka kwenye kata 48 za Wilayani hupo wamempongeza katibu wa  Jumuiya hiyo Angelo Madundo kwa kazi ya kuimarisha miradi mbalimbali ya Jumuiya ikiwemo Shule ya Sekondari Mkinga ambayo inadaiwa awali miradi hiyo ilikuwa ikilegalega.



 Naye katibu wa Jumuiya hiyo Angelo Madundo awali kabla ya uchaguzi huo aliwaambia Wajumbe hao kuwa uongozi unaochaguliwa utaenda kusaidiana na CCM kuhakikisha dola inaendelea kushikiliwa na Chama cha Mapinduzi na siyo vinginevyo.


Madundo amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ipo imara na inafanya mambo mengi hivyo lazima wapatikane Viongozi ambao watakaomsaidia kwa dhati ili Taifa lizidi kusongambelea kimaendeleo .

          

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI