Header Ads Widget

UVCCM KIBAHA MJINI WAMCHAGUA KAZEMBE

 


RAMADHAN Kazembe amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kibaha Mjini baada ya kumwangusha mwenyekiti aliyekuwa anatetea nafasi yake Godlove Rwekaza.


Katika uchaguzi huo Kazembe huku Rwekaza aliyepata kura 84 kati ya kura 316 ambapo msimamizi wa uchaguzi huo Katibu wa UWT Mkoa Fatuma Ndee alisema kuwa kura nne ziliharibika.


Ndee alimtangaza Nancy Matta kushika nafasi ya tatu kwa kupata kura 55 ambapo Mjumbe wa UVCCM wilaya kuwakilisha mkutano Mkuu Mkoa kuwa ni Valentine Mbawala.


Alisema kuwa nafasi ya mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ni Jonas Ngwesa na mjumbe wa mkutano mkuu CCM wilaya Happiness Eustace huku nafasi ya wajumbe wa Baraza la vijana wilaya Ally Gombati, Benjamin Mjata, Ashura Thomas, Mwasiti Nzota na Abuu Matumla.


Kazembe aliwaasa wanachama wa Jumuiya hiyo kujituma na kuwa wazalendo wakati wote kwenye kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi ili kujiwekea akiba ya kuaminika kwenye nafasi za Uongozi.


Naye Katibu wa UVCCM Kibaha Mjini Amina Makona alishukuru na kuwataka waliochaguliwa kuendelea kujituma kuwa wabunifu na utumishi uliotukuka na wale ambao hawafanikiwa kushinda wasikate tamaa kwani kumalizika kwa uchaguzi huo ni mwanzo wa chaguzi zijazo hivyo wasisite kuendelea kujitokeza kwenye chaguzi mbalimbali.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI