NA TITUS MWOMBEKI, Matukio Daima App Kagera.
KAULI hiyo imetolewa na Mkuu wa Kagera, Albert Chalamila wakati akizungumza na makundi mbalimbali likiwemo shirikisho la umoja wa machinga (SHIUMA) pamoja na Jukwaa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi katika kikao maalumu kilichofanyika katika ukumbi wa Bukoba Sekondari ulioko mjini Bukoba.
"Mheshimiwa Rais ametutuma tuje hapa tupambane, tukae,tuandike na tuone tunafanyaje kuusaidia mkoa wa Kagera kuondokana na umasikini"
Sambamba na hilo amesema kuwa serikali tayari imetoa pesa kwaajili ya kuanza ujenzi wa tawi la chuo kikuu cha Dar es Salaam katika mkoa huo ili kuweza kuchochea maendeleo.
"Vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini vimekubali kuja kuanza ujenzi wa matawi ya vyuo hapa nchini mfano chuo kikuu cha Dar es Salam na NIT, hii yote ni kuleta mzunguko wa fedha katika mkoa wetu na ili wana Kagera pamoja na mkoa huu uweze kunufaika kwa frusa zitakazotokana na vyuo hivyo"
Amewaomba wana Kagera hasa wasomi na wataalamu mbalimbali wenye mawazo chanya kufika ofisini kwake kutoa maoni na mawazo yao ambayo wanaona yanaweza kusaidia mkoa huo kupiga hatua za kimaendeleo.
Aidha ameshauri wafanyiashara kuacha utamaduni wa kufungua maduka muda umeenda kwani ni suala ambalo nalo ni kikwazo cha maendeleo.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Toba Nguvila amewasihi wananchi wa Kagera kuwa viongozi sio vikwazo vya maendeleo bali wapo kwaajiri ya kuwa daraja la maendeleo huku akiwasihi wananchi hao kuachana na mambo ya kuoneana wivu.
"Sis hatutaki kuwa kikwazo cha maendeleo bali ni daraja la maendeleo kwa wanakagera ila pia na nyie epukaneni na vivu na usuda na kujenga udamaduni wa kusaidiana ili muweze kujikwamua kimaisha"
Kwa upande wake Modest Abel ambaye ni mjasiriamali katika Manispaa wa Kagera amewaomba viongozi wa mkoa wa Kagera kutafuta namna ya kuwaunganisha vijana wa mkoa wa kagera na vijana wa nchi za jirani zinazopakana na Tanzania ili kushirikiana katika masuala ya kibiashara kama vijana wanaotoka katika ukanda mmoja wa Afrika Mashari.
0 Comments