Header Ads Widget

RAIS SAMIA ACHANGIA MIL.40 HARAMBEE KKKT MUFINDI MKOANI IRINGA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameungana na waumini wa Dayosisi maandalio ya kanisa la KKKT Mufindi mkoani Iringa  kwa kuchangia shilingi milioni 40  kwenye Harambe ya kumalizia ujenzi wa kanisa  akiwakilishwa katibu mkuu wa CCM Daniel Chongolo aliyefanikiwa  kukusanya zaidi ya shilingi milioni 220


Harambee hiyo iliyofanyika iliyofanyika Jumamosi ya Septemba 24,2022  ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserekali pamojaa na wambunge wa mkoa wa Iringa na walio njee ya Iringa ambao nao walishiriki kutoa sadaka ya kujenga nyumba ya bwana.


 Akizungumza kwenye harambee hiyo katibu mkuu wa CCM Daniel Chongolo aliwashukuru viongozi wa kanisa hilo kwa kumpa heshima ya kufanikishaa harambee hiyo kwani wako watu wengi lakini wakaona yeye anaweza kuendesha kazi hiyo


 "Niwashukuru Sana kwa kuniamini na kuona nafaa kujaa kuendesha shughuli hii ya harambee  nimshukuru Sana Mh Rais Samia Suluhu kwa kuniruhusu kuja hapa na nilipomuambia naye kanipaa salamu zenu nami nitaziwakilisha hapa"


Wakati naondoka niliendaa kuomba ruhusa kwa Mh na kumwambia nimeombwa na Wana mafinga kwenda kufanya harambee na akaniambia niwasalimie na Mheshimiwa Rais amenituma niwape shilingi milioni 40 ,anawapenda Sana na anawaomba muendelee kuliombea Taifa lenu la Tanzania"_Chongolo



Chongolo alisema kuwa katika harambee hiyo wapo marafiki zake waliomuunga mkono kwa kuchangia harambee hiyo ambao ni wabunge wa nje ya mkoa huo akiwemo pia mjumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Salim Abri Asas ambaye alichangia shilingi milioni tano taslimu.


Kwa upande wake Mkuu wa Dayosisi hiyo ya  maandalio ya kanisa la KKKT  Mufindi  Dkt. Antony Kipangula amemshukuru katibu mkuu wa CCM Daniel Chongolo  kwenye Harambe ya kumalizia ujenzi wa kanisa Hilo kwa kufanikisha kukusanya zaidi ya shilingi milioni 220 


Kipangula alimuomba Chongolo kuweza kufikisha shukrani zao kwa Rais wa Jamuhuri wa Tanzania na mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi CCM Mhe.Samia  kwa kuwaunga mkono kwenye harambee hiyo kwa kuwapa shilingi milioni 40.


"Mh katibu mkuu tunakushukuru Sana na tuomba pia utupelekee salamu kwa Mh Rais kwa kufanikisha harambee hii na mchango mkubwa mliotoa tunawashukuru Sana na tutazidi kuwaweka magotini pa Mungu ili muendelee kuiongoza nchi yetu kwa hekima na busara "

 

Awali akisoma risala kabla ya harambee hiyo kuanza  katibu wa ujenzi Herzon Myinga alisema kuwa matarajio ni kanisa hiyo kuanza kutumia Christmas  ambao lengo lao ni kukusanya shilingi millioni 250,000,00.


Alisema kuwa fedha wanazotarajia kukusanya zitafanya kazi ya kunakshi kuta za ndani na njee,ujenzi wa madhabau na vyoo vya ndani, kutengeneza na kufunga milango na madirisha pamoja na kulipa fidia kwa baadhi ya wakazi wanao zunguka kanisa hilo ili kuweza kupata nafasi ya kujenga choo pamoja na nyumba za watumishi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI