Header Ads Widget

DC NJOMBE AONYA WAZAZI KUACHA KUWALISHA KANDE WATOTO WAO KUPUNGUZA UDUMAVU

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaApp NJOMBE


Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amewataka wananchi  kuachana na mtindo wa kula chakula Cha aina moja hususani Kande wakati wote kwani kunachangia kwa kiasi kikubwa kushamiri kwa udumavu.


Kasongwa ametoa kauli hiyo akiwa katika vijiji vya Itunduma na Sovi kata ya mtwango katika ziara yake ya kijiji kwa kijiji katika halmashauri ya wilaya ya Njombe ambapo amesema kitendo cha watoto kushindia kande wakati wote kinasababisha utapimlo kwao jambo ambalo halifai katika ustawi wa watoto.



Aidha mkuu huyo wa walaya amekiri kuwa wananchi wa wilaya ya Njombe wamekuwa wachapakazi kwelikweli lakini isiwe sababu ya kuwaacha watoto wawe wanakula Cha aina moja ilihali kuna kila aina ya vyakula na matunda ambayo wengi hawayatumii kwa chakula zaidi ya biashara.


Amesema kuna haja ya kuweka msako wa ambao hawali matunda kwani mlo kamili unahusisha matunda kwa asilimia kubwa.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI