NA CHAUSIKU SAID_MATUKIODAIMA APP MWANZA.
Watumiaji wa bima ya afya wametakiwa kuachana na tabia ya kugushi nyaraka mbalimbali ili kupata viambayanishi vinavyowekwa katika vitambulisho vyao.
Hayo ameyabainishwa na Mkurugenzi wa Bima ya Afya Nchini Dk, Benard Konga kwenye kikao Cha kujadili na kupata maoni ya maboresho ya uendeshaji wa Mfuko huo.
Konga amesema kuwa wamekuwa wakiwakamata wanachama ambao wanajaribu kubadilisha nyaraka za serikali ili kupata mahali pa kuwaweka watengemezi wa pande zote mbili na wenza wao wa sio halali.
" Tunawaomba waajili mnapokuwa mnasaini fomu za kuomba vitambulisho mjilizishe kweli hao ndio watengemezi halali wa mwanachama husika.
Hata hivyo amesema miaka 14 hadi 15 iliyopita kulikuwa na wagonjwa wa Figo taktibani 234 ambapo kwa sasa hivi kuna wagonjwa wa figo wapatao 2000.
"Leo hii tukizingumzia miaka 15 iliyopita mfuko wa bima ya Afya ya taifa gharama kubwa ulikuwa kwenye ugonjwa wa maralia,na magonjwa ya kuambukizwa yanayoingia na kutoka lakini hivi sasa tunazungumzia saratani,Figo magonjwa ambayo yanakuwa kwa kiasia kikubwa,"Alisema Konga.
Mwenyekiti wa NHIF Dk, Ally Muhimbi ameshauri kuwa Kuna sababu ya kupitia upya baadhi ya kanuni ili kuweza kufanyia kazi maboresho ili yaweze kuendana na wakati na mazingira ya hivi sasa.
Kwa upande wake Meneja wa Mfuko wa Bima ya afya Mkoa wa Mwanza (NHIF) Jarlath Mushashu amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya kupanda kwa gharama kumekuwa na wimbi la udanganyifu kwa baadhi ya wanachama wa Mfuko huo hali ambayo inatishia kuhujumu mfuko huo.
Naye mmoja wa washiriki wa kikao hicho Sheikh wa Mkoa Mwanza ,Hassan Kabeke ameiomba mfuko huo kushirikiana kikamilifu na viongozi wa dini zote kwa kutoa elimu ya kujiunga na mfuko huo.
0 Comments