Header Ads Widget

TAKUKURU MBEYA WACHUNGUZA TUHUMA ZA WASIMAMIZI WA SENSA KUPOKEA RUSHWA


Na,Esther Macha,Matukio daima Media,Mbeya

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoani  Mbeya imesema kuwa inachunguza wasimamizi wawili wa Sensa ya watu na Makazi ambao wanadaiwa kuhusika kupokea Rushwa ya  sh.20,0000  kwa kila mmoja  ili wawapitishe makarani  kwenye usaili  ili waweze kushiriki  zoezi la sensa  ambalo limeanza  Agosti 23 mwaka huu .


Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkuu wa Takukuru mkoa wa Mbeya ,Maghela  Ndimbo amesema hayo wakati akitoa taarifa ya  miezi mitatu  ambayo ni April  mpaka Juni 2022 ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa  miradi  ya maendeleo inayogramu zaidi ya Bil.10 .


Aidha Ndimbo amesema kuwa  katika zoezi la usaili wa makarani wa sensa katika baadhi ya kata mkoani Mbeya kulikuwa na upendeleo  kwenye usaili wa makarani   ambapo kuna mtendaji na mkuu wa shule ambao waliwapa  upendeleo  watahiniwa  kwa maana kuwa mmoja anapewa maksi nyingi mwingine pungufu  ili kuwawezesha waliopewa maksi nyingi waweze kushinda na kushiriki zoezi hilo.


“Lakini kwa taarifa tulizopokea ni kuwa walifanya hivyo baada ya kupokea shilingi laki mbili (20,0000)kwa kila mmoja  na kwamba  bado tunaendelea kulifanyia kazi  suala hili na wasimamizi hawa tayari wameondolewa  kwenye usimamizi  huo na tumechukua hatua za awali kuhusiana na  tukio hili “amesema Ndimbo.


Aidha Mkuu huyo wa Takukuru ametaja wasimamizi hao kuwa ni Mtendaji wa Kata ya Sinde ,Hawa Kajula  pamoja na Mkuu wa shule ya msingi Mlimani , Baita Sanga ambapo wote wawili walituhumiwa kupokea rushwa  ya 20,0000 kwa kila mtainiwa ili waweze kupewa upendeleo na wapitwishwe kuwa  makarani wa Sensa  na kwamba uchunguzi wa awali ulifanyika na kubaini kuwa zoezi la usaili kuna baadhi  ya watainiwa  katika usaili uliofanywa  walitoa maksi  za pendeleo kwa watainiwa wanne  kwa swali lile lile  na majibu yale yale huku  wengine maksi za juu kwenye usaili huo  na chini  baada ysa kubaini hayo walichukua hatua za kuwasimamisha kwenye zoezi la Sensa la usimamizi kwa  kushirikiana  mwajiri.


“Baada ya kubaini hilo tulichukua hatua za kiutawala  kwa kushirikiana na mwajiri  pamoja na wasimamizi wa Sensa Mkoa na Wilaya kwa kuchukua hatua kwa  kuwaondoa  kwenye kushiriki zoezi la Sensa kwa kutokuwa wasimamizi wa Sensa ambao ni Hawa Idd na Baita Sanga  waliondolewa na nafasi zao kubadili watu wengine “amesema Mkuu huyo wa Takukuru.


Akifafanua zaidi Ndimbo amesema kuwa kwa watahiniwa ambao walipendelewa kwenye usaili wa zoezi la sensa  walinyimwa sifa za kuchaguliwa na  wale ambao walipunjwa maksi walipewa sifa za kuchaguliwa kuwa makarani wa Sensa.


“Kwa upande wa Rushwa bado hatujaweza kupata ushahidi wa wazi hili bado tunachunguza kwenye simu zao miamala iliyoingia ili tuone kama kuna  fedha ziliingia na kama tutabaini watafikishwa mahakamani ,lakini kama hatutabaini kuwepo kwa tukio la kupokea rushwa tunakusudia kupendekeza hatua za kiutawala zaidi dhidi yao kwani kitendo walichofanya kilikuwa na lengo la kuharibu zoezi la sensa, kwa maana ya kuondolewa tu hakitoshi hizi zilikuwa hatua za awali zilizochukuliwa lakini baada ya kukamilisha uchunguzi wetu tutatoa mapendekezo ya kiutawala”amesema Mkuu wa Takukuru.


Aidha Ndimbo ametoa rai kwa wadau wote wa sensa kujiepusha  rushwa na udanganyifu au kutumia nafasi ya usimamizi wa sensa kushiriki vitendo vya rushwa ,wananchi kuwa makini na mtu wa sensa anapokuja lazima awe na kiongozi husika wa eneo ili kukwepa udanganyifu ,lakini pia vifaa vyote vya  sensa walivyopewa makarani ni vema wakavitunza kwa umakini mpaka zoezi hilo litakapokamilika kwani ikibainika vimepotea zoezi zima linaharibika.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI