Header Ads Widget

SERIKALI YANUNUA TANZINITE YENYE THAMANI YA BIL. 2.24

 



Na,Jusline Marco:Simanjiro


Serikali ya nunua mawe mawili ya madini ya Tanzanite yenye thamani ya shilingi bilioni 2.24 yaliyopatikana kwa mchimbaji mdogo wa madini hayo, Anselm John Kawishe katika eneo la Mererani lilipo Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara. 


Waziri wa madini Dkt. Dotto Biteko akiwa mgeni rasmi katika ununuzi wa madini hayo amewataka wachimbaji wa madini kuendelea kafuata taratibu zote za uchimbaji na kufanya kazi kwa bidii kwa kuaminika ili kuondoa changamoto mbalimbali wanazokutana nazo 


Aidha Waziri Dkt.Biteko amesema Sekta ya madini ni sekta iliyo salama na inaongoza katika kukuza uchumi wa Taifa kutokana na ukusanyaji wa mapato makubwa ambapo ili kudhibiti utoroshwaji wa madini katika midogo ya mererani serikali kupitia wizara ya madini imeajiri majicho 8.



Kwa Upande wake mchimbaji huyo wa madini haho,Anselm Kawishe ambaye amefanya biashara ya madini ya Tanzanite na serikali ametoa shukrani zake za dhati kwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wachimbaji wadogo wa madini.


Naye Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere amempongeza bilionea mpya Anselm John Kawishe na kuahidi kushirikiana nae bega kwa bega katika mambo mbalimbali ya kukuza uchumi na anajivunia katika mkoa wake kupatikana kwa bilionea wa pili. 



Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adolf Nduguru amesema vipande hivyo  viwili vya madini ya Tanzanite vina uzito wa kilogramu 3.74 na kilogramu 1.48 ambapo kati ya madini hayo mawili,lenye uzito wa kilogramu 1.48 lina thamani ya shilingi milioni 713.8  na lenye uzito wa kilogramu 3.74 lina thamani ya shilingi bilioni 1.5 na yote kufanya kuwa na jumla ya shilingi bilioni 2.245.




Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka katika hafla hiyo amempongeza mchimbaji huyo wa madini kwa kufanikiwa kupata madini hayo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI