Header Ads Widget

RC SENDIGA AKABIDHI PIKIPIKI 7 KWA WATENDAJI WA KATA MANISPAA YA SUMBAWANGA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe.Queen Sendiga Leo (22 Agosti, 2022) amekabidhi pikipiki saba (7 ) kwa ajili ya watendaji wa Kata Mkoani Rukwa zenye thamani ya Shilingi milion 24 kwa ajili ya kuwasaidia Katika utendaji wao wa kazi ikiwa ni pamoja na kusimamia Miradi ya Maendeleo Katika kata zao na Usimamizi na Ukusanyaji wa Mapato ili kuimarisha Uhai wa Halamsahauri na utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Maendeleo.

Mkuu huyo wa Mkoa  amewapongeza Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa kuimarisha maeneo ya Ukusanyaji Mapato kwa kuhakikisha watumishi wanakuwa na vitendea kazi kwani ubunifu wa kuwagawia watendaji pikipiki utaongeza tija Katika Ukusanyaji Mapato na kuibua vyanzo vingine vya Mapato.


Sendiga ametoa wito kwa watendaji wa kata kutoa taarifa mapema za mashine za kukusanyia ambazo zina changamoto ili ziweze kutatuliwa ili halmashauri iwe na uhakika wa fedha za kutekeleza miradi.

Kuhusu miradi Sendiga amewataka wataalamu na watumishi wengine kuhakikisha Miradi inamalizika kwa muda uliopangwa kwenye mkataba ili kupisha uanzishwaji wa Miradi mingine.

Pia kuhusu Fedha za Mikopo ya vikundi wanaokopeshwa hizo fedha wapewe Elimu ili waweze kuanzisha Miradi itakayowasaidia kuinua vipato vyao na kuwapa uwezo wa kurejesha Mikopo kwa wakati.

Sendiga ametoa wito kwa kwa watendaji wa kata kuhakikisha wanatumia pikipiki walizopatiwa kwa manufaa ya umma na si kwa matumizi binafsi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya amesema mkakati uliopo ni kuhakikisha watendaji wa kata na mitaa wanapatiwa vitendea kazi ili waweze kusimamia na kuhamasisha shughuli za Maendeleo.

Mtalitinya alionya watendaji waliopatiwa pikipiki hizo kuwa wazitumie kwa kazi za wananchi na si kwenye shughuli binafsi na kuwa mfumo wa ufuatiliaji matumizi yake umewekwa vizuri.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI