Header Ads Widget

MUWSA YAENDELEA NA UJENZI WA MIRADI YA MAJI HUKU UJENZI UKITARAJIWA KUMALIZIKA SEPTEMBA MWAKA HUU


Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira Mjini MoshiInjinia wa mradi wa maji wa Miwaleni njia panda


*********

Mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira mjini moshi ( MUWSA) inaendelea na Ujenzi wa miradi ya maji ambapo mpaka ifikapo septemba mwaka huu wanatarajia kumalizika kwa miradi hiyo kwa asilimia miamoja.

Kaimu mkurugenzi wa mamlaka hiyo Edes Mushi amesema hayo wakati alipokuwa kwenye ziara na timu maalum ya menegmenti ya kutembelea na kukagua miradi hiyo.

Aidha amebainisha miradi hiyo ambayo ni mradi wa Maji ya Mabogini, ambao umekamilika kwa asilimia mia moja, na kusema pindi utahudumia vijijini vitatu vya mserekia,mtakuja na maendeleo.

"Lakini pia vilevile tuna mradi mwingine wa uviko ambao umekamilika kwa asilimia 99. ambao ni mradi wa Kimochi utakaohudumia kata ya Oldi Moshi, na maeneo karibu"Alisema Mushi.

Sambamba na hayo amesema mradi mwingine ni mradi wa Miwaleni njia panda ambao upo katika Asilimia 60; ya Ujenzi na kusema wanatarajia ifikapo septema 15 utakuwa umekamilika kwa asilimia miamoja.

Ameendelea kusema kuwa mradi wa njia panda Miwaleni umegharimu kiasi Cha sh, Bilioni mbili na milioni mia Tano.

"Mradi huo utakapokamilika utahudumia wakazi zaidi ya Elfu nane katika eneo la njia panda na pia itaongeza kiwango Cha maji katika eneo hilo kwani ongezeko la watu linakuwa kwa Kasi katika eneo hilo"Alisema.

Hata hivyo amesema eneo hilo ni Lina changamoto ya ukame na Lina uhitaji mkubwa wa maji hivyo kukamilika kwa mradi huo utaondoa changamoto ya ukosefu wa maji.

Injinia wa mradi wa njia panda Miwaleni Said Mrindoko amesema kuwa mradi huo wa Miwaleni utakapokamilika utawanufaisha wananchi wapatao elfu kumi na Saba na mia tatu thelathini na nane.

Wakizungumzia Ujenzi wa miradi hiyo wananchi mkoani hapa wamesema kuwa kukamilika kwa miradi hiyo itawasaidia kuondokana na Magonjwa Kama ya kichocho ambayo yalikuwa yakiwapata kutokana na kutumia maji yasiyokuwa salama kwa afya zao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI