Header Ads Widget

MSIMU WA PILI WA MBIO ZA KIMATAIFA ZANZIBAR 'TIGO ZANTEL 2022' KUFANYIKA AGOSTI 7

 




RAIS wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na atakimbia umbali wa Kilometa 10 katika msimu wa pili wa mbio za Kimataifa za Zanzibar zinazofahamika 'Tigo Zantel Zanzibar International Marathon'.


Wakitambulisha mbele ya Waandishi wa Habari na Wadau na wadhamini mapema jana Julai 31, Kamati ya mbio hizo ilibainisha kuwa, maandalizi yote yamekamilika na washiriki wanaendelea kujitokeza kwa kulipia usajili mtandaoni tayari kwa mbio siku ya Jumapili ya tarehe 7, mwaka huu.


Msimu wa pili wa mbio za Tigo Zantel Zanzibar International Marathon, tumekuja na vitu mbalimbali, ikiwemo mbio za Baiskeri ambapo pia washindi watapata zawadi nono, lakini pia kutakuwa na shughuli ya tamasha dogo la kuelekea mbio kuanzia Agosti 5 na 6 kuamkia Agosti 7 ya mbio.



Kwa mujibu wa Msemaji wa mbio hizo, Hassan Mussa Ibrahim amesema watu watakaofika mapema Unguja, watapata burudani maalum kwenye fukwe ndani ya mitaa ya Ngome Kongwe kwenye eneo la Urithi wa kale.


Aidha, alitangaza zawadi kwa washindi kwenye mbio hizo kuwa watapata medali na washindi wa kwanza watapata zawadi ya fedha taslimu pamoja na kulala kwenye hotel ya hadhi ha nyota Tano na mwenza wake.


"Agosti 7 ni mbio Moja tu, zitafanyika ndani ya Unguja katika eneo la Urithi wa kale, katika kuenzi Urithi na kuhimiza uchumi wa blue, mbio hizi zitaanzia eneo la Ngome Kongwe na kumalizikia hapo hapo Ngome Kongwe.


Kwa shilingi za Kitanzania elfu 35 tu (Tsh.35,000), utapata kushiriki mbio za KM 21, 10 na mbio za Baiskeri,


Lakini pia kutakuwa na mbio ndogo za watoto MITA 300. Kama haitosho, Wazee wanaruhusiwa kushiriki kwa mbio zote watakazoweza na zawadi itatolewa Shilingi 500,000" alisema Hassan Mussa.


"Malengo yetu tunataka watu waje Zanzibar, "wakumbuke", yaani waje mapema Ijumaa hadi Jumapili kwenye mbio zenyewe,


Lakini pia zawadi nono ni pamoja na 

KM 21 mshindi wa kwanza atapata Milioni 2.5 pamoja na vifaa vya kukimbilia kutoka maduka ya Just fit, lakini kwa mshindi wa pili atapata Milioni 2, na wa tatu atapata Milioni Moja.


Kwa upande wa washindi wa mbio za KM 10, mshindi wa kwanza atapata Milioni 1.5, na w pili milioni Moja na wa tatu atapata Laki Saba, 


Pia kwa washindi wa mbio za KM 5, watazawadiwa mshindi wa kwanza Milioni Moja, wa pili Laki Tano na wa tatu, atapata Tsh Laki tatu." Alisema Hassan.




Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani,Robert Kasulwa alisema kampuniya Tigo ambayo inafanya kazi Tanzania nzima pamoja na Visiwani Zanzibar,  amewwaomba waendeleaje kuiamini na kuitumia kwani ina huduma bora kwa wateja wake.


"Kwa kutumia Ulimwengu wa kidigitali, katika ushiriki wa wakimbiaji wote Watakaoshiriki wataweza kulipia mbio zao kwa njia ya Lipa kwa simu, ama kwa kutumia App ya TigoPesa,


Kwa wale wa lipa kwa simu watatumia namba ya 5121222, na hapo utafuata maelezo na kisha kulipia hii ni bila makato ya zaida," alisema Kasulwa.




Kwa upande wa Meneja masoko wa duka la Just fit, ambalo linajihusisha na vifaa vya michezo, Jabir Jabir alisema kuwa,  wataendelea kukuza sekta ya michezo kupitia mbio ambazo zitasaidia kukuza uchumi wa blue Visiwani Zanzibar.


"Maduka yetu ya Just fit, yapo na vifaa vya kutosha, watu wote wanakaribishwa kununua vifaa vya Michezo.


Lakini pia kit za mbio zote zinapatikana na mnakaribishwa sana kwenye maduka yetu yote hapa Dar, maduka yako wazi kila siku za wiki." Alisema Jabir.


Kamati kuu ya mbio hizo hivi karibuni ilitangaza rasmi kuingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya huduma za mitandao ya simu ya Tigo & Zantel, kwa mkataba mnono wa Billion 1.5.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI