Matukio Daima App Mwanza
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt Fiderice Mafumiko amefanya Mkutano katika Ukumbi wa TMDA na Waandishi wa habari mkoa wa Mwanza kuhusu Usimamizi na Udhibiti wa Zebaki Nchini.
Mafumiko amesema, Sheria inaagiza kila anayejihusisha na kemikali ikiwemo Zebaki anapaswa kujisajili na Mkemia Mkuu wa Serikali ambaye ndiye Msajili wa kemikali za Viwanda na Majumbani,
Aidha amesema, hadi kufikia Agosti 22 mwaka huu,Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inazitambua kampuni kumi ( 10 ) ambazo zilikidhi na kutimiza matakwa ya sheria , na hivyo kujisajili.
Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt.Fiderice Mafumiko akazitaja kampuni ambazo tayari zimekidhi na kutimiza matakwa ya sheria na kusajili ni, Tri star Ltd,Waswa Co.Ltd,Kadula & Kapata Co.Ltd,Mhange Sungwa Maduhu,Jema Chemucals Co.Ltd,Machugu Investment,Joma Enterprise,Mwiwa Co.Ltd,African Albinus Laboratories na Angelus Albninus Antony
Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt.Fiderice Mafumiko amewataka wadau wote wanaojihusisha na Zebaki ikiwemo watumiaji ambao hawajasajiliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wafuate taratibu za sheria na kanuni katika ununuzi, uuzaji, utumiaji na usambazaji wa kemikali hiyo
Mkemia Mkuu wa Serikali,Dkt Fiderice Mafumiko,ametoa rai kwa umma na yeyote ambaye ana lengo la kujihusisha na zebaki, Serikali haitasita kuchukua hatua za kali za kisheria kwa wahusika ambao awqatakuwa wamesajiliwa na Mkemia Mkuu wa Serikali.
0 Comments