Header Ads Widget

MGOGORO WA WANANCHI NA KAMPUNI YA MECHANDISE MBIONI KUMALIZIKA.

 


NA MATUKIODAIMAAPP

MGOGORO uliokuwepo baina ya wananchi na kampuni Mechandise Enterprise Ltd ambayo ilishinda kesi mahakamani juu ya eneo ambalo wananchi walilivamia unakaribia kuishi baada ya wananchi hao kuridhia kulipia gharama za ardhi na kuepusha nyumba zao kubomolewa.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde akizungumza kwenye kikao cha mtaa huo alisema kuwa baada ya hukumu ya mahakama kutoka kampuni hiyo ilitaka kubomoa nyumba zilizojengwa lakini baada ya mazungumzo baina ya uongozi wa Wilaya na Halmashauri waliomba asibomoe ila alitaka walipimie gharama za maeneo waliyoyachukua.


Munde alisema kampuni hiyo ilitaka walipe kila mita mraba kiasi cha shilingi 15,000 lakini wakaeleza kuwa gharama ya mita za mraba kwa eneo hilo kwa bei ya soko ni shilingi 5,000 kwa eneo la makazi na 6,000 kwa eneo la biashara huku wananchi wakiomba kulipa 4,000.


Aidha alisema kuwa ombi la wao kulipia shilingi 4,000 kwa mita za mraba atalipeleka kwa mkuu wa Wilaya ambaye aliagiza Halmashauri waende kulipatia ufumbuzi jambo hilo pamoja na wamiliki wa eneo hilo ili kufikia maridhiano.


Akizungumza kwenye mkutano huo moja ya wananchi hao kabla ya kufikia makubaliano ya kulipia gharama ya shilingi 4,000 kwa mita za mraba Innocent Kimaro alisema kuwa wao wanaomba wapunguziwe gharama hizo za ardhi kwani wao waliuziwa kwa kutapeliwa madalali.


Akizungumza kwenye mkutano huo moja ya wananchi hao kabla ya kufikia makubaliano ya kulipia gharama ya shilingi 4,000 kwa mita za mraba Innocent Kimaro alisema kuwa wao wanaomba wapunguziwe gharama hizo za ardhi kwani wao waliuziwa kwa kutapeliwa madalali.


Naye Asha Mgiti alisema kuwa wanaomba kufikiriwe kwani walitapeliwa na wametumia gharama kubwa kendeleza maeneo hayo pia walipe kwa awamu kwani maisha yao ni ya kawaida na hawana uwezo mkubwa.


Kwa upande wake Mwasiti Said alisema kuwa wao kama akinamama wana mzigo mkubwa wa kulea familia hivyo wanaomba serikali iwafikirie juu ya gharama za kumiliki ardhi hiyo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI