Baadhi ya Makarani wa Sensa wilayani Magu mkoani Mwanza wameomba zoezi hilo kuongezwa muda badala ya siku saba liweze kufikia siku kumi kutokana na baadhi ya kaya kuwa na idadi kubwa ya watu na kupelekea katika maeneo mengine kuchukua takribani zaidi ya masaa mawili.
Ombi hilo wamelitoa wilayani humo mbele ya mkuu wa wilaya ya Magu Salum Kalli wakati akifatilia hilo zoezi kwa ukaribu katika kata mbalimbali za wilaya hiyo.
Nao baadhi ya wakazi wilayani Magu wamelipongeza zoezi hilo huku wakiomba liongezewe muda ili wananchi waweze kutoa taarifa zao kwa usahihi zaidi.
Mkuu wa wilaya ya Magu Salum Kalli amesema,zoezi hilo litafanyika kwa uangalifu mkubwa na usahihi katika maeneo yote yakiwemo ya visiwani
Aidha Mkuu wa wilaya hiyo Salum Kalli amehesabiwa zoezi hilo nyumbani kwake Ikulu ndogo wilayani humo.
0 Comments