Header Ads Widget

MAKARANI 2 WANACHUNGUZWA NA JESHI LA POLISI KWA VISHIKWAMBI SIMIYU

Na Bahati Sonda, Matukio DaimaAPP,Simiyu.

Makarani wawili wa Sensa katika Kata ya Lamadi Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, wanachunguzwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za wizi wa vishikwambi vya sensa.


Hayo yamebainishwa mapema leo na Mkuu wa Wilaya ya Busega Gabriel Zakaria wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuwataja makarani hao Saphina John na Yona Mwalongo na kusema kuwa kwa pamoja wameibiwa vishikwambi hivyo majira ya tisa usiku wa kuamkia Agosti 26, mwaka huu wakiwa wamelala ndani ya nyumba katika Mji wa Lamadi.


Zakaria amesema kuwa ingawa makarani hao wanadai walifunga mlango baada ya kuingia kulala, lakini kwenye nyumba  waliyolala hakuna sehemu palipovunjwa, na hivyo kuagiza polisi kuwachunguza kwa uzembe uliosababisha upotevu wa mali ya umma.


Aidha akizungumzia maendeleo ya zoezi la sensa ya watu na makazi wilayani humo ni mazuri na kuwahakikishia wananchi wa wilayani humo kuwa wote watahesabiwa huku akisisitiza kuwa zoezi hilo litakamilika na  litamalizika kwa wakati.

        

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI